Tuesday, August 27, 2013
UGONJWA WA KUDUMAA WAMTESA MTOTO WA MIAKA 14 AONEKANE MZEE WA MIAKA 110
MTOTO wa miaka 14 anasumbuliwa na ugonjwa wa kuduma 'progeria', hali inayopelekea mwili wake kuonekana kama mzee wa miaka 110. Mtoto huyo aliyetambulika kwa jina la Ali Hussain, anayeishi nchini India anaonekana kama mzee wa miaka 110 kutokana na tatizo hilo linalomfanya akue kwa haraka kuliko kawaida.
Ugonjwa huo unaonekana kuitesa zaidi familia yake ambapo hadi sasa mtoto huyo ameshuhudia dada zake pamoja na kaka zake watatu wamefariki kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa huo.
Imeripotiwa kuwa watu wanaosumbuliwa na ugonjwa huo hawawezi kuishi zaidi ya miaka 14 huku wakiwa wanasumbuliwa na tatizo la macho pamoja na moyo Hussain bado kwa upande wake hajakata tamaa ya kuishi.
"Ninamatumaini ipo dawa ya tatizo langu na ninatamani sana kuishi siogopi kifo lakini wazazi wangu wanateseka sana juu yangu naumia kwani sitaki kuwabebesha mzigo wa maumivu wazazi wangu"
Tatizo hilo linaonekana ni la kurithi ndani ya familia yao ambapo baba mzazi wa mtoto huyo Nabi Hussain Khan (50) aliweka wazi kuwa kama wangeambiwa mapema na daktari juu ya ugonjwa huo wasingeendelea kuzaa.
Ripoti hiyo imedai kuwa waliendelea kuzaa kwa matumaini kuwa wangepata mtoto asiye na tatizo na ndipo walipompata Sanjeeda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment