Rapper Fat Joe ameanza kutumikia kifungo chake cha miezi minne alichohukumiwa baada ya kukutwa na hatia ya kushindwa kulipa kodi. Joe aliamua kuwaaga mashabiki wake kwa kutumia ukurasa wake wa Twitter, ikionyesha kuwa ameamua kwenda kuripoti mwenyewe jela ya Federal Detention Center, Miami nchini Marekani.
June 24 Joe alihukumiwa kifungo cha miezi 4 jela kwa kushindwa kulipa deni la kodi zaidi ya dola milioni 1 kwa kipindi cha miaka miwili 2007 na 2008, ambapo kifungo hicho kinaambatana na faini ya dola 15,000 pamoja na usimamizi maalum wa mwaka mmoja baada ya kutoka jela
No comments:
Post a Comment