WAKAZI wa Mivinjeni Kurasini wanaotakiwa kuhama kupisha mradi wa uwekezaji wa EPZ wamefunga barabara kuishinikiza Serikali kuwalipa hundi zao na si viwanja.
Hali hiyo ilijitokeza jana Dar es Salaam Majira ya Saa tano asubuhi ambapo wananchi walijipanga barabarani na kuzuia magari kupita kuishinikiza serikali kuwalipa fidia ili waweze kuondoka katika eneo hilo.
Akizungumza na gazeti hili Katibu anayefutilia malipo ya wakazi hao Judith George alisema kuwa wakazi hao wamelala barabarani kutokana na serikali kuwapiga dana dana kulipwa hundi za nyumba zao ili waweze kuhama.
Alisema kuwa Viongozi wa Serikali pamoja na Mwekezaji (EPZ) walifika katika eneo hilo March 13 mwaka huu na kufanya mkutano na wananchi kuhusu uwekezaji katika eneo hilo.
Alisema kuwa Mwekezaji huyo alipozungumza nao walikubali kuhama kupisha ujenzi wa kiwanda katika eneo hilo la Mivinjeni na aliahidi kuwalipa fedha zao ili waweze kutafuta sehemu nyingine.
Aliongeza kuwa mwekezaji huo alifuatana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka na kuahidi wakazi hao kuwapatia Viwanja mbadala katika eneo la Kigamboni Uvumba Kibanda.
Alisema kuwa baada ya hapo serikali ilishirikiana na Wilaya ya Temeke kufanya tathimini April mwaka huu ya nyumba zote za wakazi hao na kuweka x.
"Baada ya tathimini Mkuu wa Wilaya ya Temeke kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali wa serikali kwa na mwekezaji walifanya tena tatahimini na kubaini kuna nyumba 60 zina matatizo eneo la Shimo la Udongo Kurasini na kufanikiwa kuokoa sh Bilioni 1.4zilikuwa za usanii.
Aliongezea kuwa baada ya kufanyiwa tathimini walitangaziwa kwamba Agosti 26 mwaka huu wafike wilayani kwa jili ya kuchukua Hundi zao, lakini walipofika waliambiwa zoezi la utoaji hundi limesitishwa.
Hata hivyo alisema kama zoezi la ulipaji wa fidia limesitishwa kwa nini hawakutangaziwa kama walivyofanya mikutano mara ya kwanza ya kuambiwa eneo hilo linahitajika na mwekezaji.
Naye Mkazi Mwingine wa eneo hilo Mgeni Juma alisema serikali imejaa usanii tu kutokana na mwekezaji kutoa fedha za kulipwa lakini wao wanasitisha bila kutoa taarifa kwa wananchi.
Alisema kuwa kama serikali hiyo ikicheza 2015 hawaweze kupiga kura kutokana na kudanganya wananchi, tusije tukafanyiwa kama wakazi wa Kipawa walivyokuwa wanadanganywa mpaka leo.
Naye Rodi Panjo mkazi wa kurasini alisema walipotangaziwa hundi zitaanza kutolewa August 26 alisafiri kutoka Mbeya kuja kuchukua hundi yake lakini alipofika zoezi limesitishwa na ukizangatia nalala nyumba za wageni fedha ya kulipa nitapata wapi.
Mkazi mwingine Gerad Mahinya alisema biashara zao zimefungwa kutokana na nyumba hizo kuwekwa alama ya x hali ambayo hawajui hatma ya maisha yao.
"Wakazi wengi wameshahama kutoka maeneo hayo na wengin walikopa kutoka benki mbalimbali na kutafuta maeneo mengine ya kukaa huku wakitegemea kupata fedha zao ili kulipa madeni ,"alisema.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Temeke Engelbert Kiondo aliwataka wakazi hao kuwa na subira na kufika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya saa nane ili kupata majibu ni lini watapewa hundi zao.
Hata hivyo aliwataka wakazi hao kuwa wavumilivu na kuachia magari yaweze kupita ili alhamisi atawasilina na Waziri wa Ardhi aweze kwenda kuzungumza nao katika ofisi za serikali za mtaa wa kurasini.
No comments:
Post a Comment