Thursday, August 15, 2013

KONTENA LA PEMBE ZA NDOVU LARUDISHWA KENYA TOKA SINGAPORE

Kontena linaloaminika kubeba pembe za ndovu limerudishhwa mjini Mombasa baada ya mamlaka kulinasa nchini Singapore, liliripoti gazeti la Daily Nation la Kenya siku ya Jumanne (tarehe 13 Agosti).
SOMA ZAIDI NDANI...
"Kontena hilo lilikuwa miongoni mwa yaliyonaswa mapema na kurudishwa Kenya. Lakini kwa namna fulani likatoweka," alisema Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Kenya (KWS) Arthur Tuda. "Kupitia juhudi zetu na maafisa wenzetu wa usalama wa kigeni, tulilikamata tena na, hivi ninavyozungumzwa, linatarajiwa kuwasili Mombasa wakati wowote."

Makontena yaliyobeba pembe za ndovu yaliyokusudiwa kwenye Malaysia yalikamatwa bandarini Mombasa mwishoni mwa Julai na mwanzoni mwa Agosti. Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA), Mamlaka ya Bandari ya Kenya na KWS wanayatafuta mengine.

Majangili wawili na askari wawili wa wanyamapori wameuawa mwezi huu katika juhudi za kupambana na ujangili, alisema Tuda.

KWS, KRA na polisi pia wanashuku ushiriki wa maafisa wa juu katika ujangili na magendo ya pembe za ndovu, wakiwemo wafanyabiashara wawili kwenye mkoa wa Pwani, mbunge muhimu kwenye bunge la Kenya na gavana mmoja wa Bonde la Ufa. Watu hao wamehusishwa na kontena moja la pembe za ndovu lililokamatwa kwenye bandari ya Mombasa mwezi uliopita.

No comments:

Post a Comment