Wednesday, July 24, 2013

RWANDA YASAIDIA WAASI M23


Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limeikosoa serikali ya Rwanda na kusema kuwa,  serikali ya Kigali imekuwa ikiwaunga mkono waasi wa M23 wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Taarifa ya Human Rights Watch imeongeza kuwa, Rwanda ingali inawaunga mkono waasi hao wa M23 ambao wamehatarisha usalama katika maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Hii si mara ya kwanza kwa Rwanda kutuhumiwa kwamba, imekuwa ikiwaunga mkono waasi wa M23; tuhuma ambazo imekuwa ikizikanusha mara kwa mara.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imewatuhumu waasi wa M23 kuwa wametenda jinai za kuwauwa watu 13, kubaka wanawake 7 na kupora mali za watu wiki iliyopita katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

 Lambert Mende Omalanga Waziri wa Habari wa Kongo amesema kuwa, ushahidi unaonesha kuwa, kundi la M23 limefanya jinai kadhaa katika mji wa Kiwanja katika jimbo la Kivu Kaskazini.


No comments:

Post a Comment