Mtoto wa
miaka 11 ambaye ni shabiki wa soka amevunjika mkono wa kushoto baada ya kupigwa
na mpira wa shuti kali alilopiga mchezaji maarufu duniani Cristiano Ronaldo.
Kwa mujibu
wa mtandao wa habari wa televisheni ya Sky, kijana Charlie Silverwood
amevunjika sehemu mbili katika mkono wake wa kushoto baada ya kiki hiyo ya
umbali wa yadi 35.
Hata baada
ya kuumia kijana huyo hakuwa tayari kuondoka uwanjani kwaajili ya matibabu
ambapo timu yake ya Bournemouth ilipokuwa inacheza mechi ya kirafiki na Real
Madrid jumapili na kubaki kwa kipindi cha dakika 84 zilizokuwa zimebaki.
Baada ya
kufanyiwa xray alipopelekwa hospitali baada ya kuisha mechi, mtoto huyo
alionekana kuvunjika mara mbili mkono wake.
“Ni namna ya
ajabu sana mtu unavyoweza kuvunjika mkono” alisema “lakini nakubali kuwa ni
bora kuvunjika kwa sababu hiyo kuliko kuvunjika kwa kuanguka toka kwenye mti
kama ilivyowahi kumtokea baba yangu”
“usingetegemea
hii kumtokea mtu yeyote. Kama nisingeinua mkono wangu wa kushoto juu na
kujaribu kuzuia mpira ule basi ungetua usoni na ningeweza kupoteza jino la
mbele”
Baba wa
mtoto huyo Lee, ambaye pia ni shabiki wa Bournemouth alisema “ dakika moja
tukimuangalia Ronaldo amesimama na mpira, na dakika iliyofuata mpira ulikuwa
unamfuata Charlie”
Lakini
haikuwa taarifa mbaya sana kwani Charlie aliambulia jezi ya Real Madrid iliyosainiwa.
Ronaldo, 28,
aliifungia timu yake magoli mawili. Timu hiyo ilimtumia Charlie jezi kupitia mkongwe
wa timu ya Bournemouth, Steve Fletcher, kumpa pole Charlie.
Charlie pia
alipata mpira uliosainiwa na wachezaji wa timu hiyo.
No comments:
Post a Comment