Monday, July 22, 2013

MWINGEREZA MKENYA AWEKA REKODI

Mwendesha baiskeli mzaliwa wa Kenya ingawa raia wa Uingereza Chris Froome, anasema kuwa anatumai ushindi wake wa mashindano ya Tour de France utaweza kuwapa motisha vijana wa kiafrika.

Froome alishinda awamu ya miamoja ya mashindano ya Tour De France mnamo Jumapili akiwa anawakilisha Uingereza.


Froome, mwenye umri wa miaka 28,alizaliwa nchini Kenya ingawa wazazi wake ni raia wa Uingereza.

Alianza kuingia katika mashindano ya baiskeli baada ya kusaidiwa na mwendesha baiskeli mashuhuri nchini Kenya David Kinjah, na kushinda medali kwenye mashindano ya Afrika mwaka 2007 kabla ya kuhamia Uingereza.

Alisoma shule nchini Afrika Kusini.

Baada ya kushinda mashindano hayo, alisema ushindi wake unalenga kuwapa matumaini vijana hususan vijana wa kiafrika.

''Lazima waamini kuwa wanaweza kutoka nje ya bara la Afrika kuweza kujiunga na vikosi vya Ulaya,'' alisema Froome

Alishinda kwa zaidi ya dakika nne huku akishikana mikono na wenzake wa kikosi cha Uingereza.


No comments:

Post a Comment