Hatimaye msanii anayeshiriki katika video za wasanii wa muziki wa bongo fleva, Agnes Jerald 'Masogange' na mwenzake Melisa Edward, waliokamatwa Afrika Kusini na dawa za kulevya teyari walishapanda kizimbani, na kesi yao inatarajiwa tena kusomwa 13 Agoust mwaka huu nchini humo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kudhibiti Dawa za Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa aliweka wazi kuwa wanadada hao wawili teyari walishapandishwa kizimbani wiki iliyopita.
Alisema kuwa kutokana na ushahidi bado haujakamilika wadada hao wanatarajia kupanda kizimbani tena tarehe 13 mwezi Agoust mwaka huu.
Kamanda Nzowa aliweka wazi kuwa nchi zote mbili zinashirikiana kwa ajili ya kufanya upelelezi wa jambo hilo, hivyo anaamini kuwa kila jambo litaenda sawa.
"Nchi zote mbili tunategemeana kwa upelelezi, hivyo sisi huku tunafanya wa kwetu na wao wanafanya wa kwao mwishoni tunaulizana tulipofikia hivyo ndivyo tunavyofanya kazi" alisema Nzowa.
Wadada hao ambao walikamatwa nchini Afrika kusini wakitokea Tanzania wakiwa na dawa za kutengenezea dawa za kulevya ambazo zilifahamika kuwa ni Chemical bashirifu, ambazo hazina matumizi nchini.
Wasichana hao walikamatwa Julai 5, mwaka huu nchini humo wakiwa shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya sh. bilioni 6.8 wakitokea Tanzania.
No comments:
Post a Comment