Friday, May 24, 2013

YANGA : HARUNI NIYONZIMA NI MALI YETU, MWENYEWE AKILI

                                          Kiungo wa Yanga Haruni Niyonzima


HATIMAYE klabu ya Yanga jana imevunja ukimya kwa kumtambulisha mshambuliaji wake wa Kimataifa wa Rwanda Haruna Niyonzima, kuwa itamsainisha mkataba wa miaka miwili ili kuendelea kuitumikia klabu hiyo.


Yanga imevunja ukimya huo baada ya kuzuka kwa mingong'ono mingi kuwa mchezaji huo anataka kusajiliwa na Klabu ya Simba huku nayo Azam ikidaiwa kumuhitaji mchezaji huyo.

Hata hivyo bado haijabainika mkataba huo utakuwa ni wa thamani gani  watakaoingia Yanga na mchezaji huyo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Makao Makuu ya Klabu hiyo, wakati akimtambulisha mchezaji huyo kwa waandishi wa Habari, Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako alisema kulikuwa na maneno mengi kuhusu mchezaji huo na kwamba ataendelea kuwa mchezaji wa Yanga.

Alisema Niyonzima atasaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo kwa msimu ujao na kwamba mchezaji huyo bado ni mali halali ya klabu hiyo.

Kwa upande wake Niyonzima alisema yeye ni mchezaji halali wa Yanga na kwamba hiyo haimzuii kuzungumza na mtu yoyote kwa kuwa ni mchezaji.

Niyonzima ambaye ni mchezaji wa zamani wa APR na Rayon za Rwanda imedaiwa kwamba Simba  imemtengea dau la Sh. Milioni 70 kwa ajili ya kumsajili kwa msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.




No comments:

Post a Comment