Thursday, May 23, 2013
SHEHA AMWAGIWA TINDIKALI UNGUJA
SHEHA wa Tomondo Kisiwani Unguja Bw.Mohamed Omary Said amemwagiwa Tindikali na matu asiyejulikana na hivyo kupata maumivu makali sehemu za kifua na jicho .
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharibi kisiwani Unguja Mughadam Khamisi alisema tukio hilo limetokea juzi usiku nje ya nyumba ya sheha huyo, chanzo cha tukio likiwa ni baada ya sheha huyo kutoka nje ya nyumba yake kuchota maji na mharifu hakuweza kutambuliwa.
Alisema Sheha huyo amekimbizwa katika hospitali ya Mnazi mmoja kwa ajili ya matibabu ya dharula huku jeshi la polisi likiwa linaendelea na uchunguzi kwani katika uchunguzi wa awali wamefanikiwa kupata chombo kilichotumika kummwagia tindikali sheha huyo.
ALisema chombo hicho kimepatikana eneo la tukio na kimechukuliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya uchunguzi wa awali wa kitaalamu ili kubaini alama za vidole na kumpata aliyekitumia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment