Thursday, June 07, 2012

WALIOKUFA 10 WATAMBULIWA,JK AWALILIA

Na mwandishi wetu

WATU 10 kati ya 13 waliofariki dunia katika ajali ya basi la abiria aina ya Toyota Coaster namba T886 BDZ baada ya kugongana na Lori la mizigo namba T.658 ASJ mali ya kampuni ya Famari Investment ya jijiji Dar es Salaam wametambulika.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabani,Bw.Butusyo Mwambelo, alithibitisha kutambuliwa kwa marehemu hao na kuongeza kuwa bado wengine watatu hawajatambuliwa.

Kwa upande wa majeruhi sita ambao ni wanawake waliolazwa wodi namba mbili, Bw. Mwambelo alisema wanaendelea vizuri. Aliongeza kuwa majeruhi mmoja ambaye ni mwanaume anaendelea vizuri.

Aliwaja waliotambuliwa kuwa kuwa ni Immanuel Mwanjanja, Mwaniwe Focus, Lucia Livingstone (51), Lena Ngomano (49), Ngumbulu Isongole, Pius Mbeya na Mwase Pius.

Wengine ni pamoja na Bahati Jafari (33), Ernesta kikanga (62), Mwasa Diamond (40), Dereva wa Costa Mkazi wa Ilomba CCM,jijini hapa na Yerusalemu Mwakyusa (35).

Kamanda Butusyo amewataja majeruhi saba wanaoendelea na matibabu ni kuwa ni Bi. Zainabu Bahati (33), Bi. Catherine Komba(23), Bi. Neema Mwakalukwa, Bi. Veronika Charles (57), Bi. Paulina Francis (41),Bi. Esther Mgaya (21),na Bw. Ford Mwakabungu(35).

Wakati huo huo Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi na pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, kuomboleza vifo vya watu 13 waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

Katika salamu zake, Rais Kikwete amemwomba Bw. Kandoro kumfikishia salamu za rambirambi za dhati ya moyo wake kwa jamaa, ndugu na marafiki waliopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment