Na mwandishi wetu
MWENYEKITI wa Sauti ya Umma (SAU), Bw. Paul Kyara, amesema kitendo cha uamuzi wa Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi,Bw. James Mbatia, kukubali uteuzi wa Rais Jakaya Kikwete, kuwa mbunge unachangia kuua upinzani nchini na ishara kuwa chama chake kimegeuka kibaraka wa CCM.
"Uamuzi wa Bw. Mbatia unalenga kuharibu uhusiano mzuri wa chama chake na CHADEMA uliokuwa umefikiwa hadi kufikia hatua ya kumfutia kesi mbunge wa Kawe (Halima Mdee) ya kupinga matokeo ya ubunge," alisema, Bw. Kyara.
Bw. Kyara aliyasema hayo jana kupitia ujumbe wake wa simu kwa gazeti hili. Alisisitiza kuwa kama alifuta kesi hiyo bila hila ni bora akawa na hofu ya Mungu. Mwanasiasa huyo alimtaka Bw. Mbatia kuachia ngazi ya uenyekiti wa NCCR-Mageuzi vinginevyo yatamkuta yaliyomkuta Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif wa CUF.
Alimtaka Bw. Mbatia kumpongeza Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, kwa kueleza ukweli maana kuendelea kupambana naye ni kupambana na nguvu ya umma, ambayo sasa hivi Mungu ameleta uamsho wa kitaifa na wananchi wanataka mabadiliko na si vinginevyo

No comments:
Post a Comment