Monday, April 02, 2012

WABAHA’I MASHUHURI WALIOFUNGWA IRAN

Jumapili tarehe 1 Aprili huweka alama ya siku 10,000 ambazo viongozi wabaha’i wa awali 7 wamekaa gerezani kati yake kipindi chote ambacho wamekuwa wakinyimwa haki kwa mujibu wa wafungwa chini ya sheria na taratibu zao wenyewe za Iran.


Kabla ya kuwa kwao chini ya ulinzi mnamo 2008, wajumbe hawa saba walikuwa wajumbe wa kamati maalum ngazi ya kitaifa, kundi ambalo lilishughulikia mahitaji ya kiroho na kijamii ya jamii ya wabaha’i wa Iran ndani ya Iran. Wao ni Fariba Kamalabadi, Jamaloddin Khanjani, Afif Naeimi, Saeid Rezaie, Mahvash Sabet, Behrouz Tavakkoli, and Vahid Tizfahm. Ms. Sabet alishikiliwa tarehe 5 Machi 2008. Washiriki wenzake sita waliwekwa chini ya ulinzi katika uvamizi wa ahsubuhi mapema majumbani mwao tarehe 14 Mei, 2008.

Kama miezi 20 baada ya kushikiliwa bila mashitaka ndani ya gereza la Evin la Teharan, kesi ilianza tarehe 12 Januari 2010. Ilijumuisha vipindi sita vifupi vya mahakama, vyote vikinyimwa mchakatao wa kisheria uliostahili. Wale saba walishitakiwa, kati ya vitu vingine, kwa ujasusi, propaganda dhidi ya jamhuri ya waislamu na uanzishaji wa utawala usio wa kisheria, mashtaka ambayo yote yalikataliwa kabisa na kwa kupambanuliwa na watetezi. Wote walihukumiwa kifungo cha miaka 20.

Mnamo Jumapili katika jitihada zilizoratibiwa na kikundi cha muungano wa haki za binadamu kwa Iran. Picha kubwa ya wale saba itaonyeshwa kwenye mabango ya kuhamishika na mazingira mengine katika baadhi ya miji mikubwa 12 ulimwenguni kote.

"Wale kati yetu wenye uwezo wa kuongea tunahitaji kuwa sauti za wale ambao wamenyamazishwa” alisema Firuzeh Mahmoudi, mkurugenzi na muazilishi wa United4Iran. “tunatumaini hiki kitendo kitaleta makinifu ulimwenguni kote kwa hali mbaya za wale viongozi saba wa baha’i gerezani, na pia kutukumbusha juu ya wafungwa wengine wote wenye dhamiri nzuri ambao wamebaki gerezani na ambao wanahitaji msaada wetu usioyumba kwa niaba yao.
 







No comments:

Post a Comment