Tuesday, March 13, 2012

Serengeti Breweries Kudhamini Maadhimisho ya Wiki ya Maji


 Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)  kuhusiana na kampuni hiyo kudhamini maadhimisho ya 24 ya wiki ya maji ambayo kitaifa yatafanyika mjini Iringa kwa kutoa shilingi milioni 300 ambapo milioni 100 zitatumika kwenye sherehe hizo na milioni 200 zitatumika katika miradi ya maji na usafi katika mikoa ya Mwanza, Kilimanjaro, Dar es Salaam na Iringa. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi huduma za maji vijijini ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya maandalizi  Mhandisi Amani Mafuru


Mkurugenzi Msaidizi huduma za maji vijijini ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya maandalizi ya maadhimisho ya 24 ya wiki ya maji Mhandisi Amani Mafuru akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)  kuhusiana na kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kudhamini maadhimisho hayo kwa kutoa shilingi milioni 300 ambapo milioni 100 zitatumika kwenye maadhimisho hayo na milioni 200 zitatumika katika miradi ya maji na usafi katika mikoa ya Mwanza, Kilimanjaro, Dar es Salaam na Iringa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa SBL Teddy Mapunda.

                                                            Picha zote na Maelezo

No comments:

Post a Comment