Meneja wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Musoffe Laurance,akimkabidhi Cheti mshindi wa kwanza waMbio za Magunia kwa wanawake, Magreth
John, aliyeibuka kidedea katika mbio hizo wakati wa Bonanza maalum la
Wafanyakazi wa PPF lililofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Ustawi wa Jamii,
Kijitonyama jijini Dar es Salaam, leo Machi 19,2016.
Mfanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, akishiriki mchezo wakukimbiza kuku, wakati wa Bonanza maalum la Wafanyakazi wa Mfuko huo
lililofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Ustawi wa Jamii,jijini Dar es
Salaam,leo Machi 19,2016.
Showing posts with label SPOTS. Show all posts
Showing posts with label SPOTS. Show all posts
Sunday, March 20, 2016
Tuesday, January 14, 2014
BREAKING NEWS: NI RONALDO NDIO MSHINDI, SIO MESS WALA RIBERY
Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Christiano Ronaldo jana usiku alinyakua tuzo ya mchezajii bora wa soka wa fifa wa mwaka 2013 na kuwashinda Lionel Mess wa Barcelona na Frank Ribery wa Bayern Munich.
Ronaldo ambaye alinyakuwa tuzo hiyo ya mchezaji bora wa dunia kwa mara kwanza mwaka 2008 alitangazwa kunyakua tuzo mwaka 2013 baada ya kupigiwa kura na makocha, manahodha na waandishi wa habari.
Kwa mujibu wa matokeo Ronaldo alipata kura 1365 akimshinda Messi aliyepata kura 1,205 na Ribery akiambulia kura 1,127.
Ronaldo ambaye alinyakuwa tuzo hiyo ya mchezaji bora wa dunia kwa mara kwanza mwaka 2008 alitangazwa kunyakua tuzo mwaka 2013 baada ya kupigiwa kura na makocha, manahodha na waandishi wa habari.
Kwa mujibu wa matokeo Ronaldo alipata kura 1365 akimshinda Messi aliyepata kura 1,205 na Ribery akiambulia kura 1,127.
Tuesday, October 15, 2013
BRAZIL KUKIPIGA NA ZAMBIA MUDA SI MREFU
Timu ya taifa ya Zambia, Chipolopolo ndani ya saa moja kutokea
sasa wataingia uwanjani kucheza mechi ya kirafiki na timu ya taifa ya Brazil. Mechi
hiyo ambayo ni muhimu kwa Zambia ikiwa ni mechi yao ya kwanza kucheza na Brazil
ambao ni mabingwa mara tano wa kombe la dunia.
“Tunawaheshimu lakini hatuwaogopi” alisema mmoja wa
wachezaji wa timu ya Chipolopolo ambao wako jijini Beijing kwaajili ya mechi
hiyo, itakayochezwa saa saba kamili saa za Zambia ambayo ni sawa na saa moja
usiku Beijing China, katika uwanja maarufu uliojengwa kama kiota cha ndege.
Huku Chipolopolo ikiwa imetolewa katima michuano ya
maandalizi ya kombe la dunia mwaka 2014, Brazil itaingia uwanjani, ikiwa ni
mechi muhimu pia kwa katika maandalizi ya michuano ya dunia.
Wednesday, August 28, 2013
ARSENAL YAFANYA KWELI
Katika mechi iliyochezwa hapo jana kwenye uwanja wa Emirates, Arsenal imefuzu kwa Ligi ya Mabingwa kwa mwaka wa kumi na sita mfululizo.
Wageni Fenerbahce walibaki nyuma tangu mechi ya awamu ya kwanza walipofungwa mabao matatu kwa bila na Arsenal.
Friday, July 12, 2013
VILABU VINNE VYAPIGWA MARUFUKU NIGERIA
Vilabu vinne ambavyo vilihusika na njama ya kupanga matokeo ya mechi vimepigwa marufuku nchini Nigeria.Katika mechi moja klabu moja iliilaza nyingine magoli 79-0 na magoli 67-0 katika mechi ya pili.
Jumla ya magoli 146 zilifungwa katika mechi hizo mbili, idadi ambayo inaingia katika vutabu vya kumbukumbu kama mechi iliyokuwa na idadi kubwa zaidi ya magoli duniani.
Klabu ya Plateau United Feeders iliilaza timu ya Akurba ili hali timu ya Polisi ya Machine FC kwa upande wake ikailaza Bubayaro magoli 67-0.
Wednesday, May 22, 2013
Thursday, May 16, 2013
BARTHEZ, CHANONGO WAITWA STARS
Katika kikosi hicho, Kim ameita wachezaji wapya sita ingawa baadhi yao wamewahi kuchezea timu hiyo, huku akiacha wengine watatu aliokuwa nao kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Morocco ambapo Taifa Stars ilishinda mabao 3-1.
TANZANIA YAJITOA COSAFA
TANZANIA (Taifa Stars) imejitoa kwenye michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA), itakayofanyika nchini Zambia kuanzia Julai 2-26 mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah alisema Stars ambayo iliingizwa katika michuano hiyo kama timu mwalikwa imejitoa kutokana na mwingiliano wa ratiba kati ya michuano hiyo na mechi za Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).
Subscribe to:
Posts (Atom)