Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Christiano Ronaldo jana usiku alinyakua tuzo ya mchezajii bora wa soka wa fifa wa mwaka 2013 na kuwashinda Lionel Mess wa Barcelona na Frank Ribery wa Bayern Munich.
Ronaldo ambaye alinyakuwa tuzo hiyo ya mchezaji bora wa dunia kwa mara kwanza mwaka 2008 alitangazwa kunyakua tuzo mwaka 2013 baada ya kupigiwa kura na makocha, manahodha na waandishi wa habari.
Kwa mujibu wa matokeo Ronaldo alipata kura 1365 akimshinda Messi aliyepata kura 1,205 na Ribery akiambulia kura 1,127.
Kwa upande wa wanawake golikipa wa Ujerumani Nadine Angerer alinyakuwa tuzo ya fifa ya mchezaji bora wa soka kwa upande wanawake huku aliyekuwa kocha wa Bayern Munich Jupp Heynckes akinyakua tuzo ya kuwa kocha bora wa dunia. (BBC)
No comments:
Post a Comment