Taarifa zilizopatikana kwenye eneo la tukio zimeelezwa kuwa Basi hilo lenye namba T930BUW aina ya Yutong lililokuwa likiendeshwa na Dereva wake ambaye
amekimbia mara baada ya ajali hiyo linakadiriwa kuwa na abiria wapatao 48 lilipata ajali hiyo jana saa 6:50 mchana wakati lilipojaribu kulipita lori hilo upande wa kulia .
Taarifa hizo ambazo pia zimethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida zinasema kuwa kitendo hicho kilisababisha kuligonga Lori hilo RAA 496N aina ya MECEDES BENZ lililokuwa likitokea Mjini Kigali nchini Rwanda kwenda Dar es Salaam likiwa na dereva wake Barimana Benjamini (37) na kuanguka upande wa kulia wa Barabara na kujeruhi abiria wake .
No comments:
Post a Comment