Tuesday, January 14, 2014

LIVE APIGWA RISASI, KISA SIMU YAKE WAKATI WATU WANAANGALIA SINEMA

Aliyekuwa polisi mwenye cheo cha kapten ambaye kwa sasa ni mstaafu anashikiliwa na polisi kwa kuwapiga risasi watu wa wili siku ya jumatatu (jana) wakiwa kwenye ukumbi wa sinema imeripotiwa na AP.

Watu wengi hutumia simu zao wakiwa kwenye kumbi za sinema
bila kujali usumbufu wanaosababishia wenzao, file photo
Kwa mujibu wa mtandao wa Time, maofisa wa polisi huko Kaunti ya Pasco, Florida Marekani wamedai kuwa Bw. Curtis Reeves (miaka 71) alimtandika risasi Chad Oulson na mkewe Nochole wakati wakiangalia sinema Lone Survivor iliyochezwa na muigizaji maarufu Mark Wahlberg, kwa madai kuwa walikuwa wanatuma jumbe (text) fupi kwa simu zao za mkononi.

Inadaiwa Bw. Reeves alimwambia Ouslon mara kadhaa waache kutumia simu zao kwani zinasumbua watu kwa sauti na mwanga wakati sinema hiyo inaendelea.

Inaripotiwa kuwa Reeves aliwachapa risasi wawili hao katika ukumbi wa sinema uitwao Cobb Theater, ulioko Wesley Chapel huko Florida, Marekani.

Kwa mujibu wa mwendesha ukumbi huo, Oulson (miaka 43) alitandikwa risasi kifuani na mkewe kupigwa mkononi, Chad alifariki muda si mrefu baadaye akiwa hospitali. Wakati mkewe akijeruhiwa.

Ajali hiyo imeanza kuzua mjadala kuhusu usalama wa majumba ya sinema, miezi 18 iliyopita baada ya watu zaidi ya kumi kuuawa katika kumbi za sinema huko Aurora, Colorado. Muuaji James Holmes aliachiwa huru kwa madai kuwa ana matatizo ya akili baada ya tukio hilo mwaka jana


No comments:

Post a Comment