Thursday, March 22, 2018
POPE FRANCIS ALAANI MATUMIZI YA MSALABA KAMA FASHION
Na Mwandishi Wetu
Immamatukio Blog.
Papa Francis amesema matumizi ya alama ua msalaba ambayo inamaanisha kuteswa kwa Yesu Kristu kama kifaa cha fashen inachangia kudharau dini. Katika hotuba yake St Peter’s Square, Vatican, Pope Francis alisema ishara za kidini zinastahili kufikirisha na kueleweka na sio kudharauliwa.
Akikumbushia maana ya msalaba Papa alisema kuwa, msalaba sio kifaa cha kuvaa ambacho wakati mwingine kinadharauliwa, bali ni ishara ya dini cha kutafakari na kuelewa. Umbo la Yesu kusurubiwa linatukumbusha kifo cha mwana wa mungu na upendo mkuu, chanzo cha maisha na wokovu wa mwanadamu wakati wote. Natazamaje msalaba? Kama kazi ya sanaa, kuona kama yenye kuvutia au la? Au natafakari ndani katika makovu ya Yesu mpaka moyoni mwake? Naangalia maajabu ya mungu akihusisha na kifo, kama mtumwa, kama mwalifu.
Maneno yake ni kioo cha yale yaliyosemwana Askofu Mkuu wa Canterbury mwaka 2013, katika mwanzo wa kitabu chake. Alipoongelea jinsi msalaba unavyotumika.
Naye Mchungaji Justin Welby aliandika kuwa kwa wale “kwa Wakristu zamani ilikuwa ni beji ya aibu. Leo inazidi kuonekana ni ishara ya urembo kuning’iniza msalaba shingoni. Kama rafiki yangu alivyozoea kusema, ni bora hata kuning’iniza kkakidani kamti kadhahabu au kiti cha umeme (kinachotumiwa kwenye hukumu ya kifo) shingoni kwako”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment