Friday, August 25, 2017

MAMBO 6 MAZITO WALIYOIBUA LHRC LEO, SAKATA LA LISSU, BOMOA BOMOA, WAKEMEA MAUAJI

Katika kuisimamia na kulinda haki za binadamu nchini Tanzania Kituo cha sheria na hakiza binadamu Tanzania LHRC, Leo wameibuka na kukemea mambo kadhaa yanayoendelea nchini kwa sasa huku wakiitaka serikali kuyafanyia kazi kwa haraka kwani kuyaacha ni kuendelea kuminya haki za binadamu nchini,

Nchini Tanzania kwa wiki kadhaa sasa kumekuwa kukiripotiwa mambo kadhaa ikiwemo Bomoa bomoa ya maeneo mbalimbali nchini kupisha shughuli za maendeeo,kamata kamata ya wanasiasa na kuminywa na democrasia nchini.Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na -------

SAKATA LA TANAPA KUJERUHI WANANCHI

Akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam Kaimu mkurugenzi wa Kituo hicho Anna Henga ameyataja mambo ambayo wameamua kuishinikiza serikali kuyaangalia kwa jicho la Tati kuwa ni pamoja na Operation inayoendeshwa na TANAPA kulinda hifadhi ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakijeruhiwa na askari wa eneo hilo akiwemo kijana mmoja ambaye wamemtaka kwa jina la Pormoson Losso mwenye umri wa miaka 23 ambaye iliripotiwa kuwa alijeruhiwa kwa risasi na askari wa TANAPA kwa madai ya kuwa eneo la hifadhi,ambapo LHRC wamelitaka shirika hilo kuhakikisha kuwa linalinda haki za binadamu wakati likiendesha mazoezi yake kwani kutokufanya hivyo ni kinyume na sheria za nchi.

BOMOA BOMOA KIMARA

Sakata lingine ambalo LHRC wamelijadili ni kuhusu Bomoa bomoa inayoendelea ikiendeshwa na TANROADS katika barabara ya morogoro kupisha upanuzi wa barabara ambapo inasadikika kuwa mpaka sasa wakazi zaidi ya elfu moja wamebaki bila makazi maalum,huku wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto ambao wamaweza kupata madhara makubwa kwa hatua hiyo.

Sakata hilo limewafanya LHRC kuitaka serikali na taasisi zake kuhakikisha kuwa wanazingatia sheria na haki za binadamu wakati wa uendeshwaji wa zoezi hilo,ili kuepuka madhara zaidi ambayo yanaweza kujitokeza.


WAKUU WA WILAYA NA MADARAKA YAO

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali zikiwahusisha baadhi ya wakuu wa wilaya kutumia nafasi zao kuwaweka ndani baadhi ya wananchi na viongozi wa kisiasa kwa makosa mbalimbali na wengine wakiwa bila makosa jambo ambalo limezua mjadala mpana nchini Tanzania.

Sakata ambalo kwa sasa limekuwa likijadiliwa sana ni kuhusu Mkuu wa wilaya ya chemba Simon Odunga kumcharaza viboko mzazi wa mmoja wa watoto walioshambulia gari lake na kuvunja vioo kwa mawe,pamoja na lile tukio la mkuu wa wilaya ya hai Gelasius Byakanwa kuagiza jeshi la polisi kumuweka ndani mwalimu Erasto Mhagama wa shule ya secondary lerai kwa kosa aliloliita utovu wa nidhamu la kushinda kutaja jina la mkuu huyo wa wilaya na kushindwa kutaja nafasi ya ufaulu wa shule hiyo kitaifa kwa mwaka 2015.

Kwa kuzingatia matukio hayo LHRC wameitaka wizara ya nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa kuwaonya wakuu hao wa wilaya kwani matukio hayo yamekuwa yakiongezeka na hakuna sheria inayowaruhusu kufanya hivyo nchini.


POLISI NA MAUAJI YA WAHALIFU

Kufwatia matukio kadhaa ya polisi kuwaua Raia ambao wamekuwa wakiripotiwa kama wahalifu LHRC imeitaka serikali kuwapa mafunzo polisi ya kuwaweka kizuizini wahalifu badala ya kuwaua kwa kuwa hakuna shEria inayoruhusu kufanya hivyo na uwezo wa kuwakamata wanao.

MIILI INAYOOKOTWA UFUKWENI

Kutokana na kuwepo kwa Taharuki kubwa miongoni mwa Taifa baada ya kuripotiwa kuokotwa ka miili ya binadamu kadhaa inayoelea katika mito na bahari ya hindi bila kujulikana ni watu gani na ni nani anayewaua huku miili hiyo ikiwa imefungwa katika viroba,kituo hicho kimeitaka Ofisi ya upelelezi wa makosa ya jinai DPP kufanya uchunguzi wa miili na matukio hayo ili kutoa taarifa sahihi ambayo itawatoa hofu wananchi,kwa kuwa vitendo vya mauaji ya kinyama kwa binadamu kama hayo ni uvunjifu mkubwa wa sheria na haki za binadamu na watanzania wana haki ya kufahamu matukio hayo yanafanywa na watu gani ili kurudisha amani mingoni mwa watanzania.

KAMATA KAMATA YA WANASIASA

Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kimeelezwa kusikitishwa kwake na vitendo vya kuminywa kwa democrasia nchini na haki za kisiasa na kiraia, ambapo hali hii imejitokeza kwa kuwanyanyasa wabunge na viongozi hasa wa vyama vya upinzani, ikiwa ni pamoja na kamata kamata ya viongozi hao inayoendelea bila kufwata sheria za nchi,misingi na haki za binadamu.

Akitolea mfano sakata la kukamatwa mara kwa mara kwa Mbunge wa singida mashariki Mh Tundu Lissu,ambapo kwa sasa amekamatwa Tarehe 22 mwezi huu akiwa mahakama ya hakimu mkazi kisutu kwa shughuli zake kwa tuhuma za uchochezi na baadae kupekuliwa nyumbani kwake.

Wabunge wengine walokumbwa na kadhia hiyo ni Ester Bulaya mbunge wa Bunda,Godbles Lema mbunge wa Arusha mjini ambaye alikamatwa kwa kosa la kuzidisha muda wa mkutano kwa dakika saba na maadae kuachiwa.

LHRC wameitaka serikali kutoa nafasi kwa vyama vyote kufanya kazi kwa usawa bila kuingiliwa kwani Tanzania ipo katika mfumo wa vyama vingi na ni haki ya kikatiba kwa wanasiasa kuendesha shughuli zao.








No comments:

Post a Comment