Friday, August 25, 2017
JAMBO LINGINE LITAKALO KUWEPO KWENYE TAMASHA LA JINSIA MWAKA HUU
TGNP Mtandao katika kutambua nafasi ya wanajamii imetoa nafasi maalum kwa watu waliofanya mambo makubwa kwenye jamii yao na mchango wao haukutambulika, hivyo watapewa nafasi ya kuadithia simulizi zao mpaka kufikia mafanikio aliyoyapata.
Hayo yalizungumzwa jana kwenye semina ya jinsia na maendeleo (GDSS) ilifanyika mapema kwenye ukumbi wa mtandao huo Mabibo jijini Dar es salaam.
Akiongoza semina hiyo afisa programu wa TGNP Mtandao Bw. Deogratius Temba alisema kuwa lengo kuu la tamasha hilo ni kusherekea mafanikio na kuangalia changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye harakati zao.
Amesema kuwa Wametoa nafasi hiyo kwa wanajamii na washiriki wa semina za jinsia na maendeleo kuwapa nafasi ya kusimulia stori za maisha yao kwa wale waliopitia magumu mpaka kufanikiwa na kutoa zawadi kwa waliofanya vizuri katika harakati za jinsia na maendeleo.
Kwa washiriki wa semina za jinsia na maendeleo na wanajamii kwa ujumla watapata nafasi ya kushiriki kwenye mjadala wa wazi na baadae kushiriki kwenye warsha ndogo ndogo zitakazofanyika kwenye tamasha hilo.
Aidha ameongeza kuwa kwenye warsha hizo kutakuwa na mada mbalimbali zinazoongoza kila warsha kama mjadala wa Maji, Elimu, Ardhi, Mazingira Madini, Mabadiliko ya tabia ya nchi, Afya na mengine mengi.
Amesisitiza kuwa warsha hizo zitaongozwa na idara mbalimbali za serikali pamoja na mashirika rafiki na Mtandao wa Jinsia(TGNP) kama TAMWA, MEWATA, WLAC, Plan International, Haki elimu, Mfuko wa wanawake, Haki ardhi, VIWATA na mashirika mengine mengi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment