Sunday, February 14, 2016

HOSPITALI YA NJOMBE YAPEWA SIKU 90 KUJIREKEBISHA

NA MAGRETH KINABO 
MAELEZO
Uongozi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Njombe umepewa muda wa siku 90 kurekebisha mapungufu ya utoaji wa huduma za afya, lazima hospitali hiyo itafungwa. Kauli hiyo imetolewa jana jioni na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati wa akizungumza na viongozi Mganga Mkuu wa Mkoa, Samwel Mgema nana Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Imelda Mwenda na watumishi wa hospitali hiyo.

Dkt.Kigwangalla alitoa agizo kufutia ziara yake ya ukaguzi wa hospitali , vituo vya afya na zahati ili kuweza kubaini changamoto na mafanikio waliyoyapata baada maagizo mbalimbali kutolewa na Serikali. Miongoni mwamaagizo hayo ni uboreshaji wa huduma kwa kuwepo na vifaa tiba na vya maabaraza kisasa, dawa za kutosha, kuaanzamalipo ya mtandao.

Katika ziarahiyo Naibu Waziri huyo alibaini kwamba hospitali hiyo haina baadhi ya vifaa vya maabara, ambavyo nimuhimu kwa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali,ikiwemo mashine ya CT-Scan nakuwepo kwa vifaa vibovu ambayo havijafanyiwa matengenezo, ukiwemo mfumo mbovuwa ukusanyaji taka ngumu na nyepesi.

“Sijaridhishwana uendeshaji wa hospitali hii na utoajiwa huduma zinazotolewaa ninakuagizaMganga Mkuu wa Wilaya John Luanda)kurekebisha mapungufu yaliyopo baada ya miezi mitatu nitarudi nikuta hudumabado hairidhishi nitakifunga kituo.,” alisema Dkt.Kigwangalla.

Aliongezakuwa akikuta huduma hadhirishi atafunga hospitali hiyo licha ya kuwa yaSerikali, hivyo hatasubiri kutumbuliwa jipu. Dkt. Kigwangallaaliutaka uongozi wa hospitali hiyo kuandaa mpango kazi na mkakati wa kuboresha mapungufu yaliyopokatika hospitali hiyo na kuuwasilisha kwake.Aliutakauongozi wa hospitali huo kujenga chumba cha upasuaji cha wakina mama na watoto.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa Njombe, Mgema alisema watatekeleza maagizo hayo, 





No comments:

Post a Comment