Friday, February 12, 2016

DEO MWANAMBILIMBI WA KALUNDE BAND ATIWA MBARONI

Na Mwandishi Wetu

Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam imewakamatwa watu mbalimbali kwa makosa tofauti tarehe 10 Februali mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari jiji Dar ea Salaam jana Kaimu Kaminishina wa Uhamiaji Mkoa wa Dar ea Salaam John Msumule alisema kuwa watu waliokamatwa ni Abdulahi Mberwa Mtanzania mwenye umri wa miaka 37 mkazi wa Zanzibar.

Mberwa alikamatwa kwa kosa la kujihusisha na biashara ya kusafirisha binadadamu na kutoa nyaraka za uongo za wasichana wawili aliotaka kuwapeleka Uarabuni kufanya kazi za ndani ili kuwapatia paspoti za Tanzania.

Wasichana hao wametwaja kuwa ni Asma Halfe Mkenyenge miaka 26 mkazi wa Tandika na Nyamizi Halfa Kambunga miaka 31 mkazi wa Mbagala misheni Jijini Dar es Salaam.

Wengine waliokamatwa ni Deogratius Mwanambilimbi{PICHANI JUU} miaka 43 ambaye ni Mmiliki wa bendi ya Kalunde kwa kosa la kuwafanyisha kazi bila vibali vya ukaazi Kashama Alan Mulumba na Mwenebantu Kibyabya Michel wakazi wa Congo ambao nao wamekamatwa.

Watumiwa hao wanategemea kufikishwa mahakamani hivi karibuni na Msumule amewataka Watamzania wote kufichua watu wanaoishi hapa nchini bila vibali.

No comments:

Post a Comment