Meneja Masoko wa Airtel Bi Anethy Muga akionyesha moja ya tangazo la ongezeko la muda wa masaa ya vifurushi vya Airtel yatosha wakati wa kutangaza muda mpya wa kuisha kwa vifurushi vya Airtel yatosha kwa siku kuwa ni masaa 25. Yaani masaa 24 ya siku ongeza saa moja.
Airtel Tanzania imeendelea kutimiza dhamira yake ya kujali wateja wake kwa kuboresha vifurushi vyake vya huduma ya Airtel Yatosha hivyo kuvifanya kuwa bora, vya ushindani na gharama nafuu nchini.
Akiongea kuhusu kuboreshwa kwa huduma hiyo, Meneja Masoko wa Airtel Bi, Aneth Muga alisema "huduma yetu ya Airtel Yatosha inaendelea kukidhi mahitaji ya Wateja wetu kwani vifurushi tunavyotoa sasa vya Airtel Yatosha vya siku kwa shilingi 500 tumeongeza muda wake wa kutumika zaidi ukilinganisha na vifurushi vingine vinavyotolewa sokoni
Bi. Muga alisema sambamba na hili vifurushi vya Airtel Yatosha vinamuwezesha mteja kupiga simu kwenda mtandao wowote ule nchini wakati wowote masaa 25 yaani mteja anafaidika na vifurushi hivi kwa masaa 24 na 1 la nyongeza.
Kikubwa na kizuri zaidi bado pia mteja anapojiunga na vifurushi hivi anapata nafasi ya kuingia kwenye droo ya promosheni yetu kabambe ya Airtel Mkwanjika na kujishindia pesa taslimu hadi sh. Milioni moja"
Kujiunga na vifurushi mbalimbali vya Airtel yatosha mteja anatakiwa kupiga *149*99# na kisha kuchagua kifurushi kinachokithi mahitaji yake. Airtel yatosha inapatikana katika vifurushi vya siku, wiki au mwezi.
No comments:
Post a Comment