Kampuni ya kurekodi musiki ya Jay Z (PICHANI AKIWA NA RITA ORA) imempeleka mahakamani mwanamuziki Rita Ora ikimtaka alipe jumla ya pauni za Uingereza milioni 1.6 kwa kuvunja mkataba na kushindwa kutengeneza rekodi alizo ahidi.
Kesi hiyo imefunguliwa New York ikiwa ni wiki sita baada ya msanii huyo raia wa Uingereza kuishitaki Roc Nation jijini Los Angeles nchini Marekani. Kwa mujibu wa mtandao wa Sky News, Ora amedai kuwa alitengwa na watendaji wakuu na kwamba mkataba aliosaini mwaka 2008 akiwa na umri wa miaka 18 ulivunja sheria za Jimbo la California.
Msanii huyo ambaye pia ni jaji wa kipindi maarufu cha X Factor, aliwahi kutoa albamu moja tu akiwa chini la kampuni hiyo, albamu hiyo ikiwa na jina lake mwenyewe iliyotoka mwaka 2012.
Kampuni ya Jay Z, Roc Nation imedai kutumia dola za kimarekani milioni 2.4 kwaajili yake na kwamba haikuchoka kumtanganza kama mwanamuziki kwa kuwekeza mamilioni ya dola katika masoko, kurekodi muziki na gharama nyingine ambazo ni chanzo na mwongozo wa Bi.Ora mpaka kufikia ngazi ya mafanikio aliyonayo.
Hata hivyo, albamu ya pili haikufanikiwa pamoja na kwamba imedaiwa kuwa Ora alisaini mkataba wa kuzalisha albamu 5. Katika gazeti la New York Post ukurasa wa sita ulimkariri mwanasheria wa Ora, Howard King akisema “Jay Z mwenyewe alimuahidi Rita uhuru kamili, jambo ambali bado hatua za kukamilishwa.
“Tunaamini kuwa wasambazaji wa Roc Nation, Sony Music, wameitaka Roc Nation kufungua kesi hii ili wabaki na haki zote mpaka hapo watakapomalizana na Sony”
No comments:
Post a Comment