Tuesday, February 02, 2016

WHATSAPP NDIYO 'HUDUMA BORA' KIMATAIFA (BBC)

Image copyright GettyImage caption Huduma ya WhatsApp

Huduma ya simu za rununu ya kutuma ujumbe WhatsApp kwa sasa inatumiwa na takriban watu bilioni moja kila mwezi kulingana na Facebook. Huduma hiyo inayomilikiwa na Facebook, imeishinda huduma nyengine ya kutuma ujumbe ya Messenger ambayo hutumiwa na wateja milioni 800 kila mwezi.

Kampuni hiyo imesema kuwa ujumbe bilioni 42 na video milioni 250 hutumwa kwa kupitia huduma ya WhatsApp kila siku. lakini mchanganuzi mmoja amesema kuwa WhatsApp bado inakabiliwa na ushindani mkubwa katika masoko mengine.

''Kuna masoko makubwa ambapo WhatsApp haitawali," alisema Jack Kent,mchanganuzi wa rununu katika kampuni ya IHS.Image copyright ReutersImage caption WeChat

WeChat nchini Uchina ina zaidi ya wateja milioni 500, huku Line ikiwa na umaarufu Japan nayo Kakao Talk ikiwa maarufu Korea Kusini. Lakini WhatsApp ndio huduma iliofanikiwa zaidi kimataifa. Umaarufu wake unajengwa na kuwa hudumu ya mawasiliano pekee ambayo inatoa huduma kwa malipo ya chini na inaaminika sana.

Huduma nyengine zinaangazia sana fedha na michezo lakini WhatsApp inawavutia wengi kwa kuwa inatoza ada ya chini na sasa imeondoa kabisa ada yake ya kila mwaka. Facebook iliinunua huduma hiyo ya kutuma ujumbe mwaka 2014, katika mkataba uliogharimu dola bilioni 19.

''Data inayozalishwa na WhatsApp kwa facebook inaweza kuisaidia kampuni hiyo kuimarisha matangazo yake ambayo ndio biashara yake kuu'',alisema Kent.

''Facebook ilianza kuwapeleka wateja wake katika huduma ya Messenger ,iliponunua WhatsApp.Lakini kulikuwa na hatari kwamba huduma hiyo ingenyakuliwa na mpinzani wake na Facebook ingepoteza wateja wengi wanaotumia simu za rununu," alisema.

"Lakini WhatsApp bado inakabiliwa na changamoto kutoka kwa wapinzani wanaotoa huduma zoa vizuri''.

No comments:

Post a Comment