Wednesday, March 12, 2014

RONALDO NDIO MCHEZAJI TAJIRI KULIKO WOTE ULIMWENGUNI


Mtandao maarufu duniani wa soka ujulikanao kama Goal.com umetoa orodha na kutangaza kuwa klabu la Real Madrid na mshambuliaji maarufu duniani Cristiano Ronaldo kuwa ndio matajiri kuliko wote ulimwenguni katika mchezo wa soka.

Mchezaji Mpira wa Mwaka 2014 aliyechukua Lionel Messi, amepitwa katika orodha hiyo kwa utajiri wa Uro milioni 148( angalia orodha ya wachezaji matajiri 10 duniani)

Mcheza mpira aliyestaafu soka David Beckham aliongoza mwaka 2013 katika Goal Rich List, lakini baada ya kustaafu kucheza soka hana nafasi tena katika orodha hiyo.

Lionel Messi ameshika nafasi ya pili akiwa na Uro milioni 146, huku huku akifuatiwa na Eto’o mwenye Uro milioni 85, Wayne Rooney Uro milioni 84 na Kaka akifunga tano bora kwa kuwa na Uro milioni 82.

Lakini Goal imeweka wazi kuwa orodha hiyo imetumia mapato ya mchezaji anayecheza soka kama kigezo kikuu katika maisha yake yote ya kucheza soka na sio mwaka jana pekee


No comments:

Post a Comment