Ajali hiyo imepelekea ulemavu mkubwa kwa mtoto huyo ambapo
ngozi ya kidevu imeungana na kifua na kumsababishia ulemavu unaomfanya
kushindwa kula vizuri na macho kushindwa kufumba. Baba wa mtoto huyo Joseph Njavike (PICHANI AMEMBEBA MTOTO)amesema wakati wa tukio
yeye alikuwa hayupo nyumbani kwani mtoto alibaki na mama yake mzazi aitwaye
Milika Kibelege.
Milika amesema kwamba ajali hiyo ilitokea majira ya saa
mbili usiku alipokuwa anapika na yeye kupigwa na kitu kichwani kisha mtoto
kudondokea motoni nay eye kuzirai kabla ya mtoto kuokolewa na majirani baada ya
kusikia kilio kikali kutoka kwa mtoto.
ANGALIA PICHA ZAIDI. . .
Milika amesema
kuwa baada ya tukio mtoto alikuwa akipatiwa matibabu katika Zahanati ya Kijiji
cha Wanzali na kwamba yeye alikuwa akisumbuliwa na maradhi hayo hali
iliyomlazimu Dada yake kumchukua mwanae hadi Mbeya ili aweze kupatiwa matibabu
zaidi.
Kutokana na uduni wa maisha wameshindwa kufika Mbeya
kumjulia hali mtoto wao hadi walipofuatwa na Dada yake Machi 8 mwaka huu kuwa
wanahitajika Mbeya ili kibali kitolewe mtoto asafirishwe kwenda Hospitali
ya Mhimbili kwa matibabu zaidi.
Mama
Mkubwa wa Mtoto Adolotea Nyavike(PICHANI KUSHOTO) bi. Salome Kiegu(35) ambaye
alitoweka na mtoto huyo amesema anaomba radhi kwa kuondoka bila kuaga na mtoto
huyo kwani alichanganyikiwa alipoambiwa mtoto itabidi asafirishwe kwenda India
na matibabu yake yatachukua miezi sita hivyo akaona ni bora awafuate wazazi wa
mtoto huko njombe wakajadiliane
Afisa ustawi wa Jamii Mkoa wa Mbeya Thobias Mwalyego baada
ya kupokea taarifa kutoka kwa waandishi wa Habari alilazimika kwenda hadi mtaa
wa Maendeleo Iyunga ili kupata maelezo ya kina kutokana na ofisi yake kutokuwa
na taarifa zozote juu ya mtoto huyo.
Mwalyego amesema kuwa kuanzia sasa ataendelea kufuatilia
maendeleo ya mtoto huyo kuhakikisha anapatiwa huduma zinzostahili ukiwemo
msamaha wa matibabu kutoka Hospitali ya Rufaa Mbeya.
Kwa upande wa wazazi wamewashukuru wasamaria wema
waliojitokeza kuchangia matibabu ya mtoto wao na madaktari wanaofanya juhudi za
kuhakikisha mtoto huyo anapatiwa upasuaji wa haraka.
Aidha amekubali kuandamana na mwanae katika matibabu endapo
ataruhusiwa kwenda kokote na Afisa Ustawi wa Jamii alishauri pia Mama mkubwa
kuongozana na Familia hiyo kutokana na udhaifu wa mama Adorotea kwa mpenzi wangu wa maisha.”
No comments:
Post a Comment