Wednesday, March 12, 2014

HII SASA KUFURU: AMANDA AFUNGA NDOA NA MBWA, ONA STORI HII

Mwanamke mmoja raia wa nchini Uingereza ametimiza ndoto yake kwa kumpata ampendae ambaye ni mbwa wake. Huku akiwa na uhakika kuwa itabidi awe mvumilivu kwenye suala la choo, inawezekana kabisa pia akapatwa na viroboto na kupe.

(PICHA KUSHOTO: Amanda akimbusu Sheba katika sherehe ya ndoa yao)

Amanda Rodgers alifunga ndoa na mbwa wake anayeitwa Sheba katika sherehe zilizojaa mahaba iliyofanyikia Croatia. Shughuli hiyo iliudhuriwa na watu 200 na hakuna ambaye hakufurahia shughuli hiyo.

SOMA ZAIDI. . .

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 46 ambaye ni mtaliki, alivalia nguo nadhifu na za kupendeza huku mbwa Sheba akivalishwa nguo za kitamaduni za ndoa kama wanavyoonekana pichani.

Gazeti la Metro la nchini Uingereza liliripoti taarifa hiyo na kumkariri Amanda akieleza “Sheba amekuwa sehemu ya maisha yangu kwa miaka mingi, ni mcheshi na huniliwaza wakati siko vizuri. Sikuweza kufikiria kingine nacho hitaji toka kwa mpenzi wangu wa maisha.”


Amanda aliwahi kuolewa na mwanadamu miaka 20 iliyopita, lakini ndoa hiyo haikukaa muda mrefu ikavunjika. Katika kusherekea shughuli hiyo, Amanda aliandaa usiku wa music mkali huko Brixton, London na kuita usiku huo “Ajabu kuliko Mbinguni”


No comments:

Post a Comment