Wednesday, March 12, 2014

MTOTO ALIYECHINJWA NA BABA YAKE AMEFARIKI JUZI

Kahama.

Mtoto Said Siraji 13 mkazi wa majengo mjini Kahama aliyekuwa amejeruhiwa kwa kuchinjwa na baba yake mzazi amefariki dunia alipokuwa akitibiwa katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza.

Kwa mjibu wa msemaji wa familia aliyekuwa akimuuguza katika hospitali ya Bugando baada ya kuhamishiwa huko toka hospitali ya wilaya ya Kahama Bw. Hussen Idd alisema mtoto Saidi alifariki juzi saa 2 asubuhi.

Bw.Idd alisema mtoto Said aliyekuwa akisoma darasa la tatu katika shule ya msingi majengo mjini Kahama alifanyiwa unyama huo na Baba yake mzazi Bw.Siraji Salvatory 45 aliyemchija na kukata koromeo wiki iliyopita.

Alisema baada ya kuchinjwa watu wasamalia wema walimnusuru kwa kumchukua na kumkimbiza hospitali ya Wilaya ya Kahama ambako alilazwa kwa matibabu kutokana na hali yake kuwa mbaya walihamishiwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando ambako mauti yamemkuta.

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa majengo Bw.Noely Mseveni alisema mipango ya mazishi inaendelea jana nyumbani kwa mama yake mzazi Bi. Mariamu Idd kijiji cha Malunga mara baada ya mwili wa marehemu kuwasili.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya Wilaya ya Kahama Dkt. Joseph Fwoma alisema mtoto Said aliyekuwa amelazwa hapo kwa matibabu alihamishiwa bugando kwa matibabu zaidi kutokana na kuwa alikuwa amejeruhiwa vibaya kwa kukatwa koromeo na baadhi ya mishipa katika shingo yake.

Uongozi wa hospitali ya Bugando wamedhibitisha kifo cha mtoto Said aliyefariki juzi saa mbili asubuhi wakati akipatiwa matibabu kuokoa maisha yake

No comments:

Post a Comment