Wednesday, March 12, 2014

MAAJABU KWA TB JOSHUA, ALIYETUMWA KULIPUA KANISA LAKE ANASWA NA ROHO

Mtu anayedaiwa kuwa mfuasi wa kundi la Boko Haram aliyetambulika kama Mustapha anadai kutokea Adamawa, amedai yeye na wenzie wane, walitumwa kuwenda Lagos, Nigeria kulipua jengo ambalo ni kanisa maarufu kama Synagogue of All Nations.

Mustapha alisema kuwa wakiwa watano waliingia katika lango la kanisa hilo, wakamuona Mallam na kumpa bomu la mita awashikie lakini akakataa.

Kwahiyo wakaondoka kuelekea katika hoteli iliyoko karibu na kanisa hilo, lakini wakati wanapanga namna nyingine ya jinsi ya kutekeleza lengo lao, wakaona kwenye Tv(Emmanuel Tv) ambapo Mtume TB Joshua alikuwa anahubiri.

TB Joshua aliombea watazamaji na wakajikuta wanaguswa na kubadili mawazo. Wakaamua wote kutimua mbio na kuachana na lengo hilo, lakini yeye, Mustapha hakuweza kwani alikamatwa na roho.
Alieleza pia jinsi walivyoandaliwa katika mpango huo, na jinsi alivyokuwa anamuona TB Joshua katika ndoto zake akimtahadharisha kuacha kuua watu.

Angalia video hii


)

No comments:

Post a Comment