Sunday, March 16, 2014

BASI LA YANGA LIMEPATA AJALI NA VIONGOZI WAKIWEMO NDANI


Kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm akitokea dirishani baada ya ajali iliyotokea Mikese asubuh hii. Bus la timu ya Young Africans lililokuwa limebeba wachezaji pamoja na viongozi wa benchi la ufundi limepata ajali eneo na Mikese Mizani baada ya mabus yaliyokua yakitanua kuelekea mikoa ya bara kuziba njia na kusababisha kutumbukia kwenye mtaro. Katika ajali hiyo iliyotokea majira ya saa tatu na nusu asubuhi hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa na kwa sasa timu inaondoka na usafiri wa bus jingine kuelekea jijini Dar es salaam



No comments:

Post a Comment