Friday, February 07, 2014

KANISA KATOLIKI KUSHTAKIWA MAHAKAMANI, KULIPA FIDIA

Mwanaume mmoja kutoka Poland aliyedhulumiwa kimapenzi na padri mmoja akiwa mdogo ndiye mtu wa kwanza katika taifa hilo kujitokeza na kudai fidia kutoka kwa kanisa katoliki.
Mwaka uliopita, Kanisa Katoliki liliwaomba radhi watu wote waliodhulumiwa kimapenzi na mapadri kote ulimwenguni.

Hata hivyo kanisa hilo lilitupilia mbali hoja ya kuwafidia maelfu ya watoto waliodhulumiwa na makasisi na mapadri wa kanisa hilo.
Padri aliyemdhulumu mtu huyo anayefahamika kama ,Marcin K ,tayari anatumikia kifungo cha miaka miwili jela.


Mwanaume huyo anaiomba mahakama kitita cha dola elfu sitini na tano za marekani.Kesi hiyo imedhaminiwa na mashirika yanayopigania haki za kibinadamu.
Jumatano iliyopita tarehe 5 februari , Umoja wa Mataifa uliishtumu Kanisa Katoliki kwa kuendeleza sera ya kuwaficha mapadri na makasisi waliowadhulumu maelfu ya watoto ndani ya kanisa katoliki kote duniani. (BBC)

No comments:

Post a Comment