Friday, May 10, 2013
SAKATA LA CLOUDS,JAY DEE WAZIRI AINGILIA KATI
NAIBU Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla ameingilia kati ugomvi kati ya Uongozi wa Clouds Media Group na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura 'Lady Jay Dee'.
Waziri huyo ameamua kuingilia kati sakata hilo kwa kuwakutanisha, Jay Dee na Clouds ili kumaliza mgogoro uliokuwepo ambao kwa umekuwa gumzo kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa simu akiwa Dodoma, Makalla alisema malumbano hayo ambayo hayana tija isipokuwa yanakuza ambao unapoteza muelekeo wa muziki wa kizazi kipya.
"Niko tayari kukutana na pande zote mbili, uongozi wa Clouds na Jidee pamoja na Gadner, ili tukae tujadili mambo haya na tupata suluhisho la nini kifanyike," alisema Makalla.
Kutokana na malumbano hayo, Waziri huyo alisema hajafurahishwa na kitendo hicho hata kidogo kwani jambo hilo halijengi na wala halina tija kwa jamii.
Aliongezea kuwa atatumia muda mwingi ili kuwasihii wote kukutana na kuzungumza jambo na kupata muafaka kwa ajili ya kurudisha amani iliyokuwepo kwa pande zote mbili.
Clouds na Jay Dee wamekuwa wakitupiana vijembe katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kutokana na msanii huyo wa kizazi kipya, kudai kwamba kituo cha redio cha Clouds wamekuwa wakimbania kupigia nyimbo zake na pia kurusha matangazo ambayo aliyalipia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment