Taarifa zilizotufikia muda si mrefu kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)
imesitisha kwa muda na kukitaka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU)
kusitisha kufundisha na kutoa mafunzo ya Postgraduate, Masters na PhD katika
kampasi ya Dar es Salaam, Tanzania.
Hatua hiyo ni kuanzia leo, kutokana na kutokuwa na lecturers wakutosha na wenye sifa zinazostahili kufundisha program hizo.
Taarifa imetolewa na Katibu Mtendaji wa TCU, pia KIU imeamriwa kuzungumza na kushirikiana vizuri na wanafunzi wote waliodahiliwa katika kozi zilizotajwa hapo juu ili wahamie kwenye vyuo vingine vyenye idhibati ya kutoa mafunzo hayo.
“Tume haitatambua shahada yeyote ya uzamili au uzamivu itakayotolewa na chuo hicho ambao watasoma katika kampasi ya Dar es Salaam, Tanzania.
“Chuo cha KIU Kampasi ya Dar es Salaam kina ithibati na kitaendelea kutoa mafunzo ya shahada ya kwanza (Bachelors), Diploma au vyeti zilizopitishwa na TCU kwa mujibu wa Ithibati husika tuu,” imesema sehemu ya taarifa iliotolewa na Katibu Mtendaji wa TCU.
Uamuzi huo umefikiwa na tume hiyo katika mkutano wake wa hivi karibuni uliofanyika jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment