MENEJA wa msanii wa muziki wa kizazi kipya Judith Wambura 'Lady jay Dee', ambaye pia ni mume wake,
Gadna G Habashi ameingilia ugomvi uliopo kati ya mteja wake na uongozi wa Clouds Media Group.
Hatua hiyo imekuja baada ya juzi Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio, Ruge Mutahaba kukariliwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa msanii huyo amekuwa akilalamikia mambo mawili, kuhusu bendi ya Skylight
kuchukua wanamuziki kutoka Machozi Band ambayo inamilikiwa Jay Dee na matangazo yake kutorushwa hewani na kituo cha redio cha Clouds, japo alilipia sh. 240,000.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Dar es Salaam jana, Gadina alisema bendi ya Machozi bado inafanya vizuri katika tasnia ya muziki nchini na ndiyo itakayofanya shoo katika uzinduzi wa albamu ya Jay Dee, hivyo madai aliyotamka kuhusu bendi hiyo kuyumba hayana ukweli wowote.
Alisema bedi hiyo haijayumba na bado inaendelea kufanya shoo zake kulingana na ratiba zake, hivyo
ushindani ni kitu cha kawaida katika soko la muziki ubunifu ndiyo kitu ambacho wanapigana nacho, ili waendelee kuliteka soko la muziki nchini.
"Siri ya kuyumba kwa bendi ni ipi? Bendi yetu ya Machozi ipo na inafanya vizuri kwa kupiga shoo pale pale
Nyumbani na inaendelee kupata mashabiki wengi kila siku," alisema Gadna.
Alisema Jay Dee, mara nyingi anasema watu wasifikirie ni suala la wimbo kupigwa au kutokupigwa, hayo ni mambo ya kawaida lakini, wafikirie kwamba huyu mtu anaongea kutokana na uzoefu wake aliyokuwa nayo na wale watu.
Akizungumzia kuhusu kukutana kwa ajili ya kufanya majadiliano ya wazi na uongozi wa Clouds, alisema kama walikuwa wanataka majadiliano ya wazi wangemfuata Jay Dee mwenyewe kumwambia.
Alisema awali walionesha nia ya kutaka majadiliano na Ruge, lakini ilishindikana kwa kuwa Mkurugenzi huyo hakutokea sehemu walioahidiana kukutana.
"Wakati matangazo yake hayakupigwa katika redio yake, Jay Dee alimweleza juu ya kutopigwa na walikubaliana kukutana kwa ajili ya kufanya mazungumzo sehemu inayojulikana kwa jina la Alabera, lakini siku ilipofika hawakukutana na matokeo yake wala simu hakupiga, sasa anataka mazungumzo gani tena," alisema Gadina.
No comments:
Post a Comment