Thursday, June 21, 2012

WABUNGE KUCHUANA JULAI 7


WABUNGE wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania  Simba na Yanga wanatarajia kucheza mechi ya aina yake Julai 7 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Lengo la mechi hiyo ni kuwakutanisha watanzania kuwa kitu kimoja pamoja na kuchangia mfuko wa elimu kwa asilimia 20 ya mapato yatakayopatikana siku hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari jana jijini dar es Salaam Mratibu wa mechi hiyo Juma Mbizo ambaye pia ni mkurugenzi wa ukumbi wa  Dar Live alisema, wameamua kufanya tamasha hilo ili kuisaidia serikali  kujenga mabweni ya shule kwa upande wa wasichana hapa nchini.

"Tamasha hilo litakuwa la aina yake hasa pale tutakapowaona waheshimiwa wakichuana kwa lengo la kubadilishana mawazo ya nchi kujua wapi walipo na tunapokwenda,"Alisema Mbizo.

Aliwataka wadau mbali mbali wa soka kujitokeza kwa wingi siku hiyo kushuhudia viwango vitakavyoonyeshwa na wabunge hao.

Alisema,wadau hao wajiokeze ili kushuhudia upinzani utakaonyeshwa uwanjani badala ya kusikia kupitia vyombo vya habari.

Mbali na mechi hiyo vile vile kutakuwa na pambano la ngumi ambalo litawakutanisha mabondia  Cheka na Kaseba,BOngo Muvi na Bongo Fleva,pamoja na burudani kutoka kwa wasanii wa kizazi kipya Chameleon (Uganda) na Diamond.

 

 


No comments:

Post a Comment