Thursday, June 21, 2012

BENDI YA AKUDO KUPAMBA MASHABIKI CHELSEA


BENDI ya muziki wa dansi ya Akudo Impact, inatarajia kutoa burudani kwa mashabiki wa timu ya Chelsea, nchini katika kuisherehekea kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya na Kombe la FA itakayofanyika Jumapili Msasani Beach Club, Dar es Salaam.

Mbali na bendi hiyo, wasanii mbalimbali akiwemo Shilole, Mr. Nice, Muumin Mwinjuma, Chaz Baba na Irene Uwoya watakuwepo siku hiyo kunogesha sherehe hizo.


Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu wa mashabiki wa timu hiyo nchini Clifold Ndimbo, alisema maandalizi yanaendelea vizuri na siku hiyo mbali ya kuwepo soka, pia kutakuwa na burudani nyingine.

"Maandalizi yanakwenda vizuri na kwamba tumekubaliana na wenzetu wa Akudo kutoa burudani siku hiyo, baada ya michezo kumalizika na pia watakuwepo Mr. Nice, Muumini, Chaz Baba, Shilole na Uwoya kuongeza ladha katika sherehe hizo.

"Wanamuziki hao wote ni mashabiki wa Chelsea na ndiyo maana tutakuwa nao na pia tumeamua kuweka kiingilio kwa watoto ambapo sasa watalazimika kulipa sh. 1,000 na wakubwa sh. 10,000," alisema.

Kwa upande wake Akudo Impact, kiongozi wa bendi hiyo, Christian Bella ameahidi watatoa burudani ya nguvu kwa mashabiki wenzao wa Chelsea na kwamba kinachotakiwa ni kujitokeza kwa wingi.

Alisema wataanza kufanya shoo kuanzia saa nne za usiku, baada ya michezo na burudani nyingine kumalizika na wao watahitimisha kwa kuhakikisha wanakonga nyoyo za mashabiki wenzao.

No comments:

Post a Comment