Tuesday, June 19, 2012

Vodacom na Huduma Mpya



Taarifa kwa vyombo vya Habari 

Vodacom yazindua vifurushi vipya vya intanet kwa bei nafuu. 

Vodacom TZ yazindua vifurushi vya internet  ambavyo ni rahisi na vyepesi kwa wateja wao kuelewa ili kiumarisha matumizi ya huduma za intanet nchini.                     

Mteja anatakiwa kupiga *149*01# na kuchagua aina ya huduma ya intanet anayohitaji.    

Huduma ya Facebook na Twitter kuendelea kuwa bure. 

Dar es Salaam, 18 juni 2012,

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, imezindua vifurushi vipya vya intanet ambavyo vitawawezesha wateja wake kupata huduma ya internet kwa shilingi 250 tu kwa siku. 

Huduma hiyo ya Wajanja intanet imeboreshwa zaidi ili kuwawezesha wateja kuelewa huduma za intanet na kuchagua kikamilifu huduma zitakazowafaa hivyo kuweza kuperuzi na kupata taarifa kwa kasi na kwa bei nafuu kupitia mtandao wa Vodacom. 

Hata hivyo, Vodacom ilisisitiza kuwa huduma ya kuperuzi facebook na twitter zitaendelea kuwa bure kwa wateja wote.  

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza alisema kuwa  Kampuni hiyo imerahisisha huduma hiyo kwa wateja wake ili kuwawezesha kuelewa kiasi ambacho wanatumia katika huduma za intanet, suala ambalo limekuwa kikwazo kikubwa kwa watumiaji wa intanet kote nchini.

Alibainisha kuwa Kampuni hiyo imeona umuhimu wa watoa huduma za mawasiliano kama Vodacom kuondoa utata ambao unawazuia wateja kutumia mfumo mpya  wa teknolojia ya intanet katika mawasiliano.  "Tumeiweka huduma yetu katika njia ambayo ni rahisi kwa wateja wetu kuelewa kwani tunaamini kuwa hii ni njia rahisi ya kuongeza matumizi ya intanet katika kueboresha maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Wateja wote wa malipo ya baada au ya kabla watapata huduma ya internet kwa kasi kupitia simu zao za mkononi na modem.  Aliendelea kusema kuwa kutokana na huduma hiyo mpya, sasa Wateja wa Vodacom watapata huduma isiyo na kikomo na yenye kasi kwa siku saba mfululizo kwa Sh. 10,000 au Sh. 30,000 kwa siku thelathini. 

Kuweza kununua vifurushi vya internet mteja anatakiwa kupiga *149*01# na kupata orodha ya huduma za intanet kwa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi SMS wenye neno  VODACOM INTERNET kwenda 15300 bure. 

Vodacom Tanzania  inaongoza kwa mtandao wa 3G iliosambaa zaidi nchini baada ya kuwekeza zaidi ya shilingi bilioni 2 katika kupanua miundombinu yake ya intanet, na tayari uwekezaji huo umewawezesha Watanzania kunufaika na njia mpya za mawasiliano katika kujiletea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.  

Mwisho.


No comments:

Post a Comment