Tuesday, June 26, 2012

SIMU YASABABISHA GARI KUTEKETEA KWA MOTO



Moto umeteketeza gari aina ya Mercedes Benz ML Class ambalo namba zake hazikupatikana mara moja baada ya moto kuwa mkubwa, Shuhuda wa tukio hilo alisema kuwa gari hilo lilipoteza mwelekeo na kuingia mtaroni na kusababisha gari hilo kushika moto.
Alisema dereva wa gari hilo alikuwa akiongea na simu kabla ya ajali hiyo. Ajali hiyo imetokea mchana huu katika barabara ya Kilwa eneo la Tanesco

No comments:

Post a Comment