Tuesday, June 12, 2012

MAHAKAMA KUU KUCHUNGUZA UMRI WA LULU


Na mwandishi wetu
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeamua kufanya uchunguzi wa umri wa kesi ya mWigizaji nyota wa filamu nchini, Elizabeth Michael 'Lulu' anayethumiwa kwa mauaji ya mwigzaji mwenzake, Steven Kanumba

Uamuzi huo ulitolewa jana mahakamani hapo na Jaji Fauz Twaibu na kuagiza upande wa waombaji wawasilishe ushahidi wa hati ya kiapo Juni 13, mwaka huu.

Alisema mahakamani hapo kuwa maombi yaliyowasilishwa Mahakama Kuu yaliwasilishwa kimakosa na hayakufuata taratibu za kisheria na vifungu vilivyotumika vilikosewa.

Pia alisema uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kukataa maombi ya awali ya  muombaji kufanya uchunguzi wa umri wa mshtakiwa ulikuwa ni makosa kukata maombi hayo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 25, mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa.

Kiongozi wa jopo la mawakili wanaomtetea msanii huyo, Wakili Kenedy Fungamtama alidai kuwa mteja wao ana umri wa miaka 17 na si 18, kama inavyotamkwa mahakamani.

Wakili Kibatala alisema lengo la uchunguzi huo ni ili mahakama iweze kujiridhisha kama mshtakiwa ni mtoto au ni mtu mzima kwa lengo la kujipa angalizo juu ya maslahi ya mtoto.

Mbali na Kibatala na Fungamtama, ambaye pia anaitetea Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans dhidi ya Tanesco, mawakili wengine katika jopo hilo ni Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG), Joaquine De- Melo.

De-Melo ambaye amewahi kuwa Rais TLS, pia ni mshindi wa tuzo ya Mwanamke Jasiri Tanzania ya Martin Luther King.

Jopo la mawakili hao wanaomtetea msanii huyo, linahitimishwa na Fulgence Massawe kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).





No comments:

Post a Comment