Saturday, May 19, 2018

REMA FC YATINGA FAINALI KURUGENZI CUP KWA KISHINDO, KUKUTANA NA DONGOBESH FC KESHO


Aziz Rashid wa timu ya Rema 1000 FC ya Haydom wilayani Mbulu akimiliki mpira huku Elihuruma Daniel wa timu ya Airport FC akijaribu kunyanga'anya wakati wa mchezo wao wa nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Kurugenzi Cup 2018 yanayoendelea mjini Haydom, Timu ya Rema 1000 FC imeifunga timu ya Airport Magoli 8-4 na kutinga fainali ambapo sasa itakutana na timu ya Dongobesh FC ambayo nayo imeshinda mchezo wake wa leo wa Nusu Fainali baada ya kuifunga timu ya Young Boys FC magoli 2-0

Mashindano hayo yanaandaliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga na yanafanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Haydom kwa udhamini mkubwa wa Kiwanda cha maziwa cha ASAS cha mkoani Iringa na Benki ya CRDB.

Mchezo wa Fainali utafanyika kesho kwenye uwanja wa huohuo kwa kuzikutanisha timu za Dongobesh FC na Rema 1000 FC ambapo pia kutakuwa na burudani mbalimbali za ngoma za asili wakiwemo pia wachekeshaji MC Pilipili na Katarina wa Karatu.


Aziz Rashid wa Rema 1000 FC ya Haydom Mbulu akimiliki mpira huku Elihuruma Daniel wa timu ya Airport FC akijaribu kunyanga'anya huku kiatu kikiwa kimechomoka mguuni wakati wa mchezo wao wa nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Kurugenzi Cup 2018 yanayoendelea mjini Haydom


Kocha wa timu ya Rema 1000 FC Bw. Jared Ochieng akiwaelekeza wachezaji wa timu yake kwa kuchora chini kutokana na makosa waliyokuwa wakisababisha katika mchezo huo wakati wa mapumziko.


Bw.Samson Madawabora ambaye ni Daktari katika Hospitali ya Haydom na mmiliki wa timu hiyo akiwapongeza wachezaji wake mara baada ya kutinga fainali ya michuano hiyo leo.




Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga pamoja na baadhi ya viongozi wa halmashauri hiyo wakifuatilia mchezo huo.


Wachezaji wa timu ya Dongobesh FC na Young Boys FC wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa pili wa nusu fainali uliochezwa leo kwenye uwanja wa shule ya Msingi Haydom.


Kikosi cha timu ya Young Boys FC kikiwa katika picha ya pamoja.


Kikosi cha timu ya Dongobesh FC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.


Wachezaji wa timu ya Dongobesh FC na Young Boys FC wakichuana vikali katika mchezo wao wa nusu fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Haydom leo.




Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga kulia akiwa na Mchekeshaji MC Pilipili wakifuatilia mchezo wa Nusu fainali kati ya timu ya Dongobesh FC na Young Boys FC.


Mchekeshaji MC Pilipili akitangaza mchezo wa nusu fainali kati ya timu ya Dongobesh FC na Young Boys FC wakati ulipokuwa ukiendelea kwenye uwanja wa shule ya Msingi Haydom.




Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga akiwa na mtangazaji wa Radio Clouds Jacob Mbuya wakishuhudia mchezo huo.




Mashabiki wa timu ya Dongobesh FC wakimbeba juu juu golikipa wao anayejulikana kwa jina la Mapilau mara baada ya kuibuka washindi wa mchezo huo na kutinga fainali.










Mashabiki mbalimbali wakiwemo akina mama wakiwa wamefurika uwanjani kushuhudia mchezo huo.





No comments:

Post a Comment