Monday, September 18, 2017
FEZA YAKABIDHI VYETI KWA WASHINDI WA GENIUS CUP FINAL 2017
Mkurugenzi wa shule za Feza, Ibrahim Yunus, akikabidhi cheti kwa Baqirhasan Murtaza jana baada ya kuibuka mshindi wa pili katika mashindano ya Genius Cup Final 2017, huku aliyeshika nafasi ya kwanza ni Yusuf Abdallah (Hayupo pichani) kutoka shule ya sekondari ya Shamsia, iliyoko Mbweni Dar es Salaam, Baqirhasan ni mwanafunzi kutoka shule ya sekondari ya Almuntazir ya jijini Dar es Salaam, mashindano hayo yaliyoandaliwa na shule Feza na kufanyika katika shule ya Feza International iliyoko Salasala, Kata ya Kunduchi, Kindondoni, mkoani Dar es salaam tarehe 16/09/2017
Katika picha ya pamoja ni washindi wa mashindano ya Genius Cup Final 2017 kwa shule za msingi (Junior) na shule za sekondari (Senior) wote kutoka mkoa wa Dar es Salam, kushoto mwisho ni Mkuu wa Shule ya Feza Boy's, Simon Albert na kulia mwisho ni Mkurugezi wa shule za Feza Ibrahim Yunus. Shindano hilo lilifikia hitimisho jumapili tarehe 17/9/2017, ambapo washindi walikabidhiwa vyeti pamoja na zawadi zikiwemo fedha taslimu. Shindano hilo lilihusisha mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Mtwara, Pwani, Arusha, na Zanzibar.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali nchini wakishiriki mashindano ya Genius Cup Final 2017 yaliyoandaliwa na kufanyika katika shule ya Feza International, iliyoko Salasala, Kata ya Kunduchi, Kindondoni, mkoani Dar es salaam jumamosi tarehe 16/09/2017 ambapo washindi watatu wamepeta vyeti na zawadi ya shilingi laki tatu, laki mbili na laki moja na nusu kwa washindi wa kwanza mpaka wa tatu. Mashindano hayo yameandaliwa kwa lengo la kukuza vipaji katika masomo ya hisabati na sayansi nchini yenye lengo la kuondoa dhana ya kwamba masomo hayo hayawezekani. (Picha zote na Mpiga Picha Wetu)
IMEANDALIWA NA BLOG YA IMMAMATUKIO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment