Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya Microsoft imewaka hadharani rasmi mipango yake ya kutoa huduma ya Microsoft Cloud kwa mara ya kwanza kutokea kwenye vituo vyake barani la Afrika. Uwekezaji huu mpya ni hatua kubwa ya kampuni hiyo katika kuwezesha kila mtu na makampuni yote ulimwenguni kutambua fursa mbalimbali zilizopo Afrika katika mfumo wa kidijitali.
Kwa mujibu wa taarifa ya Microsoft iliyotolewa na shirika la abari la APO iliyotolewa tarehe 18/05/2017, ilieleza kuwa kampuni hiyo inatanua uwekezaji katika miradi iliyopo na kwamba itatoa huduma mbalimbali pamoja na cloud, Microsoft Azure, Office 365, na Dynamics 365 kutokea katika vituo vyake vya data vilivyoko Johannesburg na Cape Town, Afrika Kusini ifikapo mwaka 2018.
Huduma hiyo mpya yenye uwezo wa uhakika na utendaji itaongeza fursa za ukuaji wa uchumi na upatikanaji wa cloud na huduma ya internet kwa mashirka na Bara la Afrika kwa ujumla.
“Tumehamasishwa na ongezeko la mahitaji ya huduma ya cloud barani Afrika pamoja na kivutio cha fursa mpya za uchumi” alisema Scott Guthrie, Makamu wa Rais, Cloud and Enterprise Group, Microsoft Corp. “kupatikana kwa huduma hiyo Barani Afrika, kutawawezesha wataalamu kutumia ubunifu mkubwa kutengeneza Apps, wateja kubadilisha biashara zao, na serikali kutoa huduma bora zaidi kwa raia wao.”
Cloud Computing ni utumiaji wa mitandao na kuweza kufikia seva zilizo mbali ili kuhifadhi, kuendesha, na kuchakata data badala ya kuwa na computer, seva yako mwenyewe au zile zilizoko nchini kwako. Lengo la huduma hii ni pamoja na kuhakikisha usalama wa uhakika kwa watumiaji wa kompyuta na mitandao ya intaneti.
No comments:
Post a Comment