Timu ya Watumishi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakiingia uwanjani kwa maandamano wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Mei Mosi kitaifa yanayofanyika mjini Moshi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
KAMATI ya
Mashindano ya Mei Mosi ,imeonya timu za Mashirika kutumia wanamichezo
wasio watumishi (Watumishi Bandia ) katika mashindano hayo huku
ikitangaza kutoa adhabu kali kwa taasisi ama mashirika yatakayobainika
kuwatumia wachezaji hao.
Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo
ambayo hufanyika katikamkoa ambao siku kuu ya Wanyakazi Duniani
hufanyika kitaifa, timu zitakazo bainika kufanya udanganyifu zitafikwa
na rungu la kufungiwa mwaka mmoja kutoshiriki mashindano hayo pamoja na
faini ya kiasi cha sh 500,000.
Mbali na adhabu hiyo kwa timu
iliyofanya udanganyifu ,pia viongoz wa timu husika watafungiwa kwa muda
wa miaka miwili kushiriki mashindano ya Mei mosi ,adhabu itakayoenda
sambamba na nakala ya barua kwa waajili wa viongozi hao ya kuonesha
namna watumishi hao si waaminifu.
Katibu Mkuu wa Kamati ya
Mashindano hayo yanayofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu Cha Ushirika
Moshi (MoCu) baada ya kuzinduliwa jana ,Hawad Safari alisema ili kutoa
uhakiki kamati imetoa maelekezo kwa wanamichezo wafike na vitamburisho
vya kazi,Fomu inayoonesha mshahara pamoja na kadi ya bima ya afya.
Alisema
mashindano hayo yanahusisha timu kutoka katika mashirikisho manne
ambayo ni Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Uma (SHIMUTA),Shirikisho
la Michezo la Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI ) ,BAMATA
na Shirikisho la Michezo Serikali za Mitaa (SHIMISEMITA).
Safari
alisema hadi sasa jumla ya timu 14 kutoka taasisi na mashirika
mbalilimbali zimewasili mjini hapa kwa ajili ya kushindana katika
michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,Netiboli,Kuvuta kamba ,Mbio za
baiskeli ,Marathoni pamoja na michezo ya jadi kama Bao ,Drafti na
Karata.
Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano hayo
uliotanguliwa na maandamano kwa timu shiriki,Mkuu wa wilaya ya
Moshi,Kippi Warioba alisema zipo taarifa kuwa baadhi ya viongozi wa
taasisi na mashirika wamezuia kushiriki michezo hiyo licha ya kwamba
timu zao zilikwisha fanya maandalizi.
“Nivitake vyama vyama vya
wafanyakazi kufuatilia suala hili ,kwa nini wafanyakazi hawashiriki
katika michezo hasa hii ya Mei Mosi Kitaifa ….nchi yetu imekuwa haipigi
hatua kwenye eneo hili ni kwa sababu ya viongozi hawa wasiopenda michezo
mahala pa kazi”alisema Warioba.
Awali akitoa hotuba yake Kaimu
Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano hayo Joyce Benjamini alisema
Mashindano hayo yamelenga kuongeza ushirikiano mwema kwa wafanyakazi
katika maeneo yao ya kazi huku akitoa rai kwa viongozi kutenga bajeti
kwa ajili ya mashindano hayo.
Timu zinazo shiriki mashindano
hayo ni pamoja na Wizara ya Uchukuzi,Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makao
–CDA Dodoma,Ofisi ya Rais Ikulu,Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania
(TPDC) na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Timu
nyingine ni Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU),Halimashauri ya wilaya
ya Hai,Halmahauri ya wilaya ya Moshi ,Halmashauri ya Manispaa ya
Moshi,Ofisi ya katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro,Geita Gold
Mining,Mamlaka ya Hifadhi ya taifa ya Ngorongoro na TAMISEMI.
Katika
michezo ya awali timu ya soka ya TPDC ilifanikiwa kuchomoza na ushindi
baada ya kuiadhibu timu ya Halmashauri ya wilaya ya Hai kwa bao moja kwa
sifuri huku timu ya Chuo Kikuu cha Ushirika ikitakata mbele ya timu ya
Ras –Kilimanjaro kwa jumla ya ba 2 kwa 1.
Timu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakiingia uwanjani .
Timu ya Wizara ya Uchukuzi wakingia uwanjani.
Timu za Mashirika na Taasisi mbalimbali wakiwa wamebeba mabango wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano ya Mei Mosi yanayofanyika kitaifa mjini Moshi.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Mashindano ya Mei Mosi kitaifa ,Awadi Safari akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano hayo uliodfanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya Mashinano ya Mei Mosi Kitaifa ,Joyce Benjamini akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano hayo katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Mgeni rasmi katika ufunguzi rasmi wa mashindano hayo ,Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akitoa hotuba ya ufunguzi wa mashindano hayo.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba (aliyevaa suti) akiongozana na Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Mei Mosi kitaifa ,Joyce Benjamin kwa ajili ya ukaguzi wa timu zinazoshiriki mashindano hayo.
Mwamuzi wa Kike ,Salma akimtamburisha Mkuu wa wilaya timu mbalimbali zilizopo pamoja na kumkaribisha kwa ajili ya ukaguzi.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akisalimiana na wachezaji wa timu ya RAS Kilimanjaro.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akisalimiana na wachezaji wa timu ya Geita Gold Mining.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akisalimiana na wachezaji wa Netiboli wa timu ya RAS Kilimanjaro.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akipiga mpira kuashiria uzinduzi rasmi wa mashindano ya Mei Mosi kitaifa yanayofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Timu ya soka ya Geita Gold Mining wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo dhidi ya RAS -Kilimanjaro .
Timu ya soka ya RAS -Kilimanjaro kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mchezo wake dhidi ya Geita Gold Mining ,mchezo ulimalizika kwa timu ya RAS-Kilimanjaro kuchomoza na ushindi wa bao 1-0.
Kikosi cha timu ya TPDC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wake dhidi ya timu ya Halmashauri ya wilaya ya Hai.
Kikosi cha timu ya Halmashari ya wilaya ya Hai kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wake dhidi ya TPDC mchezo uliomalizika kwa TPDC kuchomoza na ushindi wa bao 1-0.
Mshambuliaji Tumaini Masue wa timu ya Chuo Kiku cha Ushirika Moshi,akijaribu kumpita mlinzi wa timu ya RAS -Kilimanjaro mchezo ambao timu ya Ushirika ilichomoza na ushindi wa bao 2-1.
Wachezaji wa timu ya TPDC na Halmashauri ya wilaya ya Hai,wakichuana vikali .
Mchezo mwingine ulikua ni netiboli ambapo ,timu zimekuwa zikichuana vikali kuwania umalkia wa mchezo huo.
Timu za TPDC na MUHAS zikimenyana katika mchezo wa kuvuta Kamba ,mchezo ulimalizika kwa TPDC kushinda mhezo huo baada ya kuwavuta wenzao kwa awamu mbili.
No comments:
Post a Comment