Na Mwandishi Wetu
Mwanamuziki mashuhuri na aliyewahi kuwa maarufu duniani,
Prince amefariki dunia. Alikutwa leo
asubuhi katika nyumba yake Minnesota, nchini Marekani, alikokuwa akiishi,
kurekodi miziki yake, alipofanyia tafrija mbalimbali, pamoja na matamasha ya
muziki
Ni miaka michache tu Prince alifanya tamasha katika eneo
lake hilo na kuonekana kwake.
Kituo cha televisheni cha Fox 9, kimemripoti Mkuu wa Polisi
wa Kautni ya Carver Jason Kamerud kudhibitisha kupokea simu kutoka nyumbani kwa
Prince ikidhibitisha kifo cha mkongwe hiyo.
“Inasikitisha kwamba nadhibitisha kifo cha mkongwe
mtumbuizaji wa kuigwa, Prince Rogers Nelson, amefariki akiwa katika eneo lake
la Paisley ambapo ni nyumbani kwake asubuhi leo akiwa na umri wa miaka 57”
msanii huyo alijipatia umaarufu mkubwa katika muziki na
kuzoa tuzo 7 za Grammy, na alitajwa na kushirikishwa (Nominations) katika tuzo
za muziki zaidi ya mara 30. Pia alishinda tuzo kubwa kuliko zote duniani za
Oscar katika kibao chake kilichotumika katika filamu ya Purple Rain.
Pince atakumbukwa sana. Ameacha alama kubwa sana katika
ulimwengu wa muziki pamoja na utamaduni wa POP, na hatosahaulika. Mungu amlaze
mahali pema peponi.
No comments:
Post a Comment