


Mwenyekiti na Msemaji wa Umoja wa wakurugenzi kutoka Uganda Bwana Dunstan Balaba Akieleza Jambo kwa Hadhara na Kukiri kushangazwa na watanzania Kuweza Kugundua Teknolojia kama hii. Pia Kumwomba Mkurugenzi wa Maxmalipo Afungue Ofisi Uganda Mapema iwezekanavyo.

Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa Kutoka UGANDA wakifuatilia Mada Kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Kampuni ya Maxmalipo Bw. Deogratius Lazari ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Maxmalipo Juma Rajabu anasema; Safari ya kuuaminisha Umma na Serikali kwamba wazawa wanaweza kubuni mbinu mbalimbali za kusaidia kuboresha makusanyo, inaenda sambamba na ufanisi mzuri uliothibitika katika kazi mbalimbali ambazo kampuni Imekua ikizifanya, Juma Rajabu ameongeza kwa kuelezea jinsi ambavyo teknolojia imerahisisha ulipajji wa bili mbalimbali Ikiwamo Luku, Kodi za TRA, Ving’amuzi na hata ukusanyaji wa mapato kwenye vivuko.

Mmoja Wa wakurugenzi kutoka Uganda Bibi Lilian Akiuliza Swali kwa Maxmalipo wakati Jumuiya hiyo ya wakurugenzi wa serikali za Mitaa wapatao 60 Kutoka Uganda leo wametembelea Ofisi za Maxmalipo Kujifunza ni jinsi Gani kampuni hii Imeweza kuugundua teknolojia inayosaidia kudhibiti makusanyo kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato katika Halmashauri za miji na majiji Nchini Tanzania.

Jumuiya ya wakurugenzi wa serikali za Mitaa wapatao 60 Kutoka Uganda wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni ya MAXCOM Africa mapema leo walipokuwa wametembelea Ofisi za Maxmalipo Kujifunza ni jinsi Gani kampuni hii Imeweza kugundua teknolojia inayosaidia kudhibiti makusanyo kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato katika Halmashauri za miji na majiji Nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment