Kenya imesema inaendela na msimamo wake juu ya suala la kurudisha
kundi la Wataiwan nchini China, tendo ambalo limechukuliwa kama mwanzo wa uhasama.
“wamekuja kutoka China na tumewarudisha China” msemaji wa
Wiziri wa Ndani Nchini Kenya, Mwenda Njoka aliiambia Shirika la Habari la
Uingereza, Reuters.
PICHA: Johnny Chiang, afisa wa chama cha Kuomintang, akionesha
video ya Raia wa Taiwan kuzuiwa na kituo cha polisi nchini Kenya, katika
mkutano na vyombo vya habari uliofanyika jijini Taipei, tarehe 12/04/2016
Taiwan imekuwa ikijitawala tokea mwaka 1949, na kujitambua
kama taifa kamili. Lakini China inakitaja kisiwa hicho kama sehemu yake. Waziri
wa Mambo ya Nje wa Kenya, Amina Mohammed, ameiambia Reuters “tunaamini sera za
‘China moja’.”
China imewekeza mabilioni ya dola nchini Kenya. Kenya
iliwazuia raia wa Taiwan pamoja na China kwa tuhuma za kuhusika na ubadhilifu
wa mawasiliano, ambapo baadhi wameonekana hawana hatia. Lakini ripoti zinazotofautiana
zimekuwa zikiibuka kuhusiana na kilichotokea tokea wakati huo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Taipei, raia 8 wa Taiwan
walirudishwa ijumaa iliyopita na wengine 37 jumanne, ikijumuisha na wale ambao
walionekana kutokuwa na hatia kwa mujibu wa mahakama.
Nairobi imedai Wataiwan 8 walirudishwa nchini China siku ya
jumatatu na wengine 16 jumanne. Wakati wanarudishwa siku ya jumanne, shirika la
Reuters liliripoti, maofisa wa Kenya walitumia mabomu ya machozi kuwalazimisha
Wataiwan kutoka kwenye vyumba vyao vya rumande kupanda ndege, Waziri wa Mambo
ya Nje wa Taiwan aliongeza kuwa mmoja wa walifukuzwa nchini Kenya ana uraia wa
Marekani. Serikali ya Marekani imedai kulifanyia kazi suala hilo.
Serikali ya China imekuwa ikieneza dhana ya utaifa wao
duniani bila kujali mtazamo wa Taiwan
No comments:
Post a Comment