Wednesday, April 13, 2016

WAFANYAKAZI AIRTEL WAINGIA MTAANI KUTOA ELIMU YA HUDUMA MPYA

Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw, Sunil Colaso akiongea na wateja wa Airtel mkoani Morogoro leo kuhusu huduma mpya ya Jipimie Yatosha yako iliyozinduliwa mwazoni mwa wiki hii. Airtel ilizindua huduma ya Jipimie yatosha yako ili kutoa uhuru kwa watumia wa huduma ya vifurushi vya Airtel Yatosha kutengeneza na kujipia vifurushi kadiri watakavyo. Leo hii wafanyakazi wa Airtel wote wameingia mtaani na kwenda kuwaonyesha wateja jinsi watakavyofaidi huduma hiyo. (na Mpiga Picha Wetu)



Wafanyakazi wa Airtel watambulisha huduma ya Airtel Jipimie Yatosha Yako kwa wateja wake sokoni


Kufatia uzinduzi wa huduma mpya ijulikanayo kama Airtel Jipimie Yatosha Yako kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imewatembelea wateja wake katika maeneo mbalimbali jijini Dar es saalam na kuwafikishia huduma hii mahali pao pa kazi na makazi yao lengo likiwa ni kutoa elimu jinsi gani ya kujitengenezea vifurushi vinavyokidhi mahitaji yao

Airtel Jipimie Yatosha Yako "ni moja ya kifurushi cha kibunifu zaidi kinachompatia mteja uhuru wa kujiunga na Airtel, kuchangua na kupanga matumizi yake kwa kuunda kifurushi kitakachokidhi mahitaji yake kiuchumi na kijamii.

Akiongea kuhusu zoezi hilo Mkurugenzi wa technologia ya habari wa Airtel, Bwana Frank Filman alisema “ tumeona ni vyema kupeleka huduma hii kwa wateja wetu na kuwaelekeza ni jinsi gani sasa wanaweza wajitengenezea vifurushi vya yatosha vinavyokidhi mahitaji yao. Kupitia huduma hii ya Airtel Jipimie Yatosha Yako sasa tumewawezesha wateja kununua kifurushi cha muda wa maongezi tu, au kuchanganya kifurushi cha muda wa maongezi na MB za intaneti au Muda wa Maongezi na SMS lakini pia bado wanaweza kupata vifurushi vyote yaani muda wa maongezi zaidi, SMS zaidi na MB zaidi

Wakiongea kwa nyakati tofauti mkazi wa Sinza Kijiweni na Fundi rangi bwana Hamisi Chande alisema “ hii ni habari njema kwetu wateja kwamba sasa tunaweza kujitengenezea vifurushi tunavyotaka kwani itatupa fursa ya kupata zaidi, awali nilikuwa naweza kumnunuali ndugu yangu kufurushi na kupata hadi huduma ya intaneti wakati sumu yake haina huduma hii sasa kupigia huduma hii mpya tutafaidika zaidi na pia tutaweza kupanga vyema vifurushi kulingana na matumizi yetu. Nawapongeza sana Airtel kwa kuja na huduma hii ya kisasa na kutuletea elimu huku tuliko.”

Kujiunga na kifurushi cha Yatosha na kufurahia Jipimie Yatosha Yako, wateja wanatakiwa kupiga namba *149*99# na kuchagua namba 5 ‘Jipimie Yatosha Yako’ na kutengeneza kifurushi cha chaguo lake.








No comments:

Post a Comment