Johnson & Johnson imetakiwa kuilipa dola za Marekani
milioni 72 (sawa na shilingi 156,783,600,000 za Tanzania) familia ya mwanamke
mmoja aliyepoteza maisha baada ya kupata saratani ya kizazi iliyohusishwa na
matumizi ya poda(Baby Powder na Shower to Shower) kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa Gazeti la Independent, rekodi za mahakama,
Jaji wa Makama ya Missouri alitoa hukumu iliyotaka familia ya Jacqueline Fox
ilipwe dola milioni 10(shilingi 21,775,500,000) kufidia maumivu na dola milioni
62 (shilingi 135,008,100,000)kwa kusababisha kifo.
Hii ni kesi ya kwanza kuwahi kutokea na kufanya maamuzi
dhidi ya tuhuma za bidhaa za poda aina ya talc kusabisha saratani. Kuna kesi
zisizopungua 1000 zinazohusisha bidhaa za poda ya Johnson & Johnson
zilizofunguliwa katika mahakama mbalimbali nchini Marekani zikidaiwa
kusababisha saratani.
Familia ya Fox imedai kuwa Marehemu alitumia bidhaa hizo
kwaajili ya usafi wa sehemu zake za siri kwa zaidi ya miaka 35 kabla ya
kugundulika ana saratani ya kizazi miaka mitatu iliyopita. Jacqueline alifariki
mwezi oktoba akiwa na miaka 62.
Mwanasheria wa familia ya Fox aliwaambia wanahabari “Johnson
& Johnson ilijua toka miaka ya 80 kuhusu athari hizo, lakini waliendelea
kudanganya jamii, na kudanganya mawakala wa afya”
Kutokana na taarifa hizo, msemaji wa Johnson & Johnson,
Carol Goodrich alisema “Johnson & Johnson imeumizwa sana na matokeo ya kesi
hiyo. Tunaungana na familia hiyo na kusikitishwa sana lakini tunaamini kuwa
ubora wa bidhaa hizo kwa miaka mingi umeshuhudiwa pia na ushahidi wa kisayansi”
No comments:
Post a Comment